Kuhusu Taizé

Jumuiya leo

Leo hii, jumuiya ya Taizé inaundwa na zaidi ya maruda mia, Wakatoliki na kutoka madhehebu mbalimbali ya Kiprotestanti, wakitoka karibu nchi therasini. Kwa uwepo wake, jumuya hii ni “fumbo la jumuiya” ambayo inataka maisha yake yawe ihsara ya maridhiano kati ya wakristu waliogawanyika.

Mabruda wa jumuiya wanaishi kutegemea kazi za mikono yao. Hawapokei misaada. Kwa namna hiyohiyo, hawapokei urithi binafsi; jumuiya huwapa masikini.

Baadhi ya mabruda huishi katika mazingira ya maskini sehemu mbali mbali duniani, kuwa mashahidi wa amani huko, pamoja na watu wenye shida. Makundi haya ya mabruda, Asia, Afrika na Amerika ya Kusini, wanashiriki hali ya maisha ya watu wanaowazunguka. Wanajitahidi kuw katika uwedp wa upendo pamoja na walio maskini sana, watoto wa mtaani, wafungwa, wanaokufa, na wote walioumizwa kwa mahusiano au waliterekezwa.

Kwa mianka mingi, vijana wamekuwa wanakuja Taizé kwa idadi kubwa zaidi kila mwaka, wanakuja kutokea kila bara kushiriki mikutano ya kila wiki. Masista wa Mtakatifu Andrea, Jumuiya ya kimataifa ya Kikatoliki iliyoanzishwa karne saba zilizopita, masista wa Polish Ursuline na masista wa Mt. Vicent wa Paulo huchukua baadhi ya majukumu yahusihanayo na kuwakaribisha vijana.

Viongozi wa Kania pia huja Taizé. Hibyo jumuiya imewakaribisha Baba mtakatifu Papa Yohane Paulo II, Maaskofu wakuu wanne wa Cantenbury, Viongozi wa makanisa ya Mashariki, Maaskofu kumi na nne wa Kilutheri wa Swedeni, na wachungaji wasiohesabika kutoka kote duniani.

Kuanzia mwaka 1962 na kuendelea, mabruda na vijana wamekuwa wanatumwa na Taizé kwenda kutembelea nchi za mashariki ya Ulaya, kwa usiri mkubwa, kutembelea wale walizuiliwa katika mipaka yao.

JPEG - 112.4 kb

Bruda Roger alifariki 16 Agosti 2005, akiwa na umri wa miaka 90, aliuawa wakati wa sala ya jioni. Bruda Alois, ambaye Bruda Roger alimteua kuwa mrithi wa nafasi yake miaka mingi iliyopita, ndiye kiongozi wa jumuiya kwa sasa.

Printed from: https://www.taize.fr/sw_article12067.html - 29 November 2023
Copyright © 2023 - Ateliers et Presses de Taizé, Taizé Community, 71250 France