Historia Fupi

Historia, mwanzo

Mambo yote yalianza mwaka 1940, akiwa na umri wa miaka ishirini na tano, Bruda Roger aliondoka Switzerland, nchi aliyozaliwa, na kwenda kuishi Ufaransa, ambapo mama yake alitokea. Kwa miaka mingi alikuwa mgonjwa, akisumbuliwa na maradhi wa kifua kikuu. Wakati wote wa kipindi hicho kirefu cha ugonjwa, wito wa kuunda jumuiya ukua ndani mwake.

Wakati vita kuu ya pili vya dunia ilipoanza, alipata msukumo kuwa, bila kupoteza wakati aanze kusaidia watu waliokua wakipitia kipind hicho cha matatizo, kama vile ambavyo bibi yake alivyofanya wakati wa vita kuu ya kwanza ya dunia. Kijiji kidogo cha Taizé, alipoweka makazi yake, kilikuwa jirani na mpaka ulioigawa Ufaransa katika pande mbili, hivyo kilikua mahali pazuri pa kuwapokea wakimbizi waliokuwa wanakimbia vita. Marafiki waliokuweko Lyon walianza kuwaelekeza Taizé, watu waliokuwa wanahitaji hifadhi.

Katika kijiji cha Taizé, kwa mkopo mdogo Bruda Roger aliweza kununua nyumba ambayo ilikua haitumiki kwa miaka mingi. Alimuomba mmoja wa dada zake, Genevieve, kuja kusaidia kutoa huduma . Kati ya wakimbizi waliowahifadhiwa walikuwamo wayahudi. Rasilimali zilikuwa chache. Hakukuwa na maji kwenye mabomba, hivyo kwa maji ya kunywa ilibidi kufuata kwenye kisima cha kijiji. Chakula kilikua cha kawaida, haswa uji uliotengenezwa kutokana na unga wa mahindi yaliyonunuliwa kwa bei nafuu katika mashine ya kusaga iliyokuwa jirani.

Katika hali ya usiri wa wale waliokuwa anawahifadhi, Bruda Roger alisali pekeyake; mara nyingi alikwenda kuimba mbali na nyumba, katika miti ili kusiwe na yeyote kati ya wakimbizi, Wayahudi au wale wasioamini ajisikie vibaya.Genevieve aliwaeleza kila mmoja kuwa, ingekuwa vyema kwa wale waliopenda kusali, kufanya hivyo peke yake chumbani kwake.

Wazazi wa Bruda Roger, hali wakitambua kuwa watoto wao walikuwa katika hali ya hatari, walimuomba rafiki wa familia yao, ambaye alikuwa Ofisa mstaafu wa kifaransa, ili awaangalie. Katika kipindi cha vuli cha mwaka 1942, aliwaonya kwamba wamefahamika walipo na hivyo kila mmoja anapaswa kuondoka haraka iwezekanavyo. Hivyo mpaka mwisho wa vita Bruda Roger aliishi Geneva na ilikuwa huko ambapo alianza kuisha maiya ya pamoja na mabruda wa kwanza. Waliweza kurudi mwaka 1944.

JPEG - 10.1 kb

Nia za mabruda wa kwanza

Mwaka 1945, wakili mmoja kijana kutoka eneo hilo alianzisha kikudi cha kuwatunza watoto yatima wa vita. Alipendekeza kwa mabruda kuwa wawapokee baadhi yao Taizé, Bruda Roger alimuomba tena dada Genevieve arudi na kuwatunza na kuwa mama yao. Siku za jumapili Mabruda waliwaalika wafungwa wa vita wa kijerumani waliokuwa wamefungwa katika kambi ililyo kuwa karibu.

Taratibu vijana wengine walifika kujiunga na kundi la awali, na siku ya pasaka 1949, Mabruda wa kwanza waliweka nia zao za kuishi maisha ya useja, ya pamoja na urahisi.

Katika ukimya wa mafungo ya muda mrefu, wakati w majira ya kipupwe ya mwaka 1952-53, mwanzilishi wa jumuiya aliandika mwongozo wa Taizé, akileza kwa kina kwa kaka zake “kitu muhimu ambacho uwezesha maisha ya pamoja”.

Printed from: https://www.taize.fr/sw_article12068.html - 11 October 2024
Copyright © 2024 - Ateliers et Presses de Taizé, Taizé Community, 71250 France