Barua 2007

Barua toka Kolkata

Miaka thelathini iliyopita, Bruda Roger alitumia muda wake kuishi huko Kolkata (Calcutta) pamoja na mabruda na vijana kutoka mabara mbalimbali, akiishi katika wilaya fukara na kushiriki katika kazi za mama Teresia za kuwahudumia watoto waliotelekezwa na wanaokufa. Alilete tena barua kwa watu wa Mungu, alifanya hazarani wakati wa mkutano wa vijana huko Notre Damae Cathedral Paris. Baadaye aliandika, taarifa kadha wa kadha na vitabu vitatu pamoja na mama Teresia.
 
Wakati kama huu mwaka 1976 ulikuwa kama mbegu ya kudumu ya uhusiano wa jumuiya yetu na wakristu wa India. Matembezi ya sehemu zote za nchi, mikutano miwili ya kimabara huko Madras na vijana kutoka India kufika Taize bila kukoma kumeonyesha hatua nyingine ya uhusiano huu. Pia kolkata iliendelea kutuonyesha watu wanosumbuka na watu wenye nyuso ambao wanatoa maisha yao kwa ajili ya wale walio fukara zaidi na hivyo kua kielelezo cha nuru.
 
Kwa hiyo nilifikiri ilikuwa muhimu kurudi Kolkata na kuandaa mkutano huko. Mkutano huo ulileta pamoja vijana 6000, wengi wao wakiwa Waasia, kuanzia tarehe 5-9 Octoba, 2006, mkutano uliiua ni jaribio la kutoa mwelekeo mpya wa "hija takatifu duniani" - kusafiri pamoja na vijana kutoka Asia ndani ya bara lao wenyewe, kuwasikiliza na kuwatia nguvu katika matumaini na matarajio yao. Barua kutoka Kolkata iliandikwa baada ya mkutano huu, ili kuwekwa hadharani katika mkutano wa Ulaya huko Zagreb.

Tunavyoendelea na "hija takatifu duniani" ambayo huleta vijana kutoka sehemu mbalimbali pamoja, hivyo tunaelewa zaidi na zaidi kwa undani kabisa ukweli huu, kila mtu hufanya familia moja na Mungu huishi ndani ya kila mtu bila ubaguzi.

Kule India, kama ilivyo sehemu nyinginezo za Asia, tumegundua ni kwa kiasi gani uhalisia umechangia uwepo wa Mungu katika uumbaji , heshima kwa watu wengine na kile kilichotolewa kwa ajili ya mtu huyo. Leo hii katika jamii zilizoendelea, ni muhimu sana kuamsha tena ule usikivu kwa Mungu na ile heshima kwa binadamu.

Kila mwanadamu ametolewa kww ajili ya Mungu. Kristo alifungua mikono yake msalabani ili kuwakusanya watu wote katika Mungu. Kama anatutuma hadi miisho yote ya dunia kuhabarisha Upendo wa Mungu, hii itafanyika katika yote kwa mazungumzo ya maisha. Mungu kamwe hatuweki katika nafasi ya kushindana na wale wasio mjua yeye.

Vijana wengi sana ulimwenguni kote wako tayari kufanya umoja wa kifamilia kuonekana zaidi. Wanajiacha wenyewe kupata changamoto kutokana na swali hili: ni kwa vipi tunaweza kuzuia aina zote za ugomvi na kubaguana; ni kwa vipi twaweza kwenda mbali zaidi ya kuta za chuki na kutofautiana? Kuta hizi ipo kati ya watu na mabara, lakini pia, kuta hizi zipo karibu sana na kila mmoja wetu, na zaidi zinapatikana ndani ya mioyo ya wanadamu. Ni jukumu letu basi kufanya uchaguzi, tuchague upendo tuchague matumaini.

Matatizo makubwa mno ya jamii nikushindwa kulea. Hivyo kwa kuchagua kupenda temetambua nafasi ya uhuru imara wa baadaye wa sisi wenyewe na kwa wote wanaotuamini sisi.

Licha ya kiasi kidogo cha werevu, Mungu ametufanya waumbaji kam yeye, hata ambapo hali ya mambo hairuhusu. Kuelekea kwa wengine, wakati mwingine kwa mikono mitupu, sikiliza, jaribu kuelewa... na tayari hali ya mkwamo inaweza kubadilika.

Mungu anatusubiri (anatungojea) wale wote walio masikini kuliko tulivyo. "Chochote ukitendacho juu ya mmoja wa hawa wadogo kuliko umenifanyia mimi." [I]

Upande wa kaskazini hivyo hivyo upande wa kusini, utofauti mkubwa huweka hai hofu ya baadaye. Baadhi ya watu wenye ushupavu hujitolea nguvu zao kubadili muundo wa kidhalimu.

Sisi sote inatupasa kujiuliza kuhusu mtindo wa maisha yetu. Inatupasa kuishi pasipo anasa (kawaida). Kwa sababu hiyo sisi itaturahisishia kwenda mbele ya wenzetu kwa moyo mkunjufu.

Siku hizi kuna mahali palipo anzishwa kwa kila mmoja kuchangia. Uvumbuzi na hakli nzuri ya mtindo wa biashara, au mikopo midogodogo, imeonyesha wazi ukuaji wa uchumi na mshikamano kwa masikini sana unaweza kwenda mkono kwa mkono. Baadhi ya watu wamehakikisha sehemu ya mapato yao yanchangia uanziswaji wa jambo kulingana na uwezo wao.

Kujitolea muda wetu ni thamani kubwa kam jamii zetu zitapata zaidi ya muonekano wa kibinadamu. Kila mmoja ajaribu kusikiliza na kusaidia angalau mtu mmoja mwingine: motto aliyetelekezwa, vijana wasio na kazi wala matumaini, watu Fulani walionyang anywa, na wazee.

Kuchagua kupenda, kuchagua matumaini. Hivyo hivyo tunavyutembea katika njia hii ya uvumilivu, tunasangazwa kwa kutambua kwamba, kabla atujafanya chochote, Mungu ametuchagua sisi sote: “Usiogope; Nimekuita wewe kwa jina; Wewe ni mali yangu. Mimi ni mungu wako, wewe unathamani kubwa mbele yangu (machoni pangu) na ninakupenda.” [II]

Katika sala, tunajiweka sisi wenyewe na wote watuaminio katika ukarimu wa macho ya Mungu.Mungu ametukaribisha sisi kama tulivyo, kwa yaliyo mazuri, lakini pamoja na migongano ya ndani mwetu na hata makosa yetu.

Injili inatuthibitishia sisi kwamba katika madhaifu yetu yanaweza yakawa ni mlango wa roho mtakatifu kuingia ndani ya maisha yetu.

Miaka thelathini iliyopita, huko Calcutta Bruda Roger aliandika: “Sala ni chanzo cha kupenda kwako. Katika utimilifu wa sifa za mtu, jitenge mwenyewe, mwili na roho.kila siku ingia ndani katika mistari michache ya maandiko matakatifu, kwa kuletwa uso na wengine, kwa bwana mfufuka. Katika ukimya, ruhusu neno hai la kristu lizaliwe nsani mwako, baadaye iliishi kwa vitendo.”

Wakati anaondoka (Bruda Roger) huko Calcutta, aliongeza kwa kusema:

“Sasa tunaondoka baada ya kutambua, katika moyo wa kuhuzunisha, mshangao wa uchangamfu wa watu, na yamethibitisha ushuhuda tofauti wa baadaye kwa kiwango cha juu kabisa. Hivyo hivyo kwa kuchangia kwa baadaye, watu wa Mungu wana uwekano ndani mwao: Kuenea toka upande mmoja hadi mwingine mwa dunia nzima, itajenga fumbo la ishirikiano katika familia ya kibinadamu. Fumbo hilo litakuwa na nguvu ya kujitangaza lenyewe, hata kutikisa maumbile yasiohamishika na kuanzisha ushirika mtakatifu katika familia ya kibinadamu.” [III]

Ombi hili la Bruda Roger ni zaidi ya hata uhusiano uliopo siku hizi. Kutawanyika toka upande mmoja hadi mwingine wa dunia, wakristu wanaweza endeleza matumaini kwa wote kwa kuanzisha maisha mapya katika habari ya kustaajabisha baada ya ufufuo wa kristo, utu wetu kamwe hauta vunjika vipande vipande.

Kwa namna gain tutakuwa mashahidi kwa Mungu wa upendo juu ya ulimwengu huu kama sisi tuaruhusu mgawanyiko kati ya wakristu kuendelea. Twende kwa ujasiri kuelekea umoja unaonekana! Wakati sisi tunapomrudia kristu kwa pamoja, wakati sisi tunaenda kusali kwa pamoja,Roho mtakatifu tayri ameshatuunganisha sisi. Unyenyekevu katika kusali, tumejifunza kujitegemea kwa kila mmoja. Je tutakuwa na ujasiri (ushupavu)wa kutenda bila kuwajali wenzetu?

Kwa kadiri tunavyomwendea kristu na injili yake, ndivyo tunavyokuea karibu na kila mmoja wetu.

Kupeana zawadi kunakuja kwa kutendeana ukarimu. Zawadi zote hizi zina umuhimu siku hizi kwa kufanua sauti ya injili kusikika. Kwa wale walioweka imani yao kwa kristu wanahimizwa kuonyesha umoja wao kwa kiwango cha juu kabisa.Na kumtukuza mungu panaweza kupenya kutoa habari njema.

Na baadaye fumbo zuri la injili linkuja kwenye maisha yetu: Nakuwa mbegu ndogo ya haradali iliyoweza kukua na kuwa mmea mkubwa bustanini ambapo ndege wa angani wanakuja kujenga viota vyao pale. [IV] Ukomavu katika kristu, tumegundua nafasi ya kuwa wawazi kwa kiwango cha juu kabisa, hata kwa wale waote wasioamwamini yeye au wenye tofauti. Kristu amakuwa mtumishi wa wote;hamdhalilishi (hamfedheshi)hata moja wetu.

Zaidi hata,siku hizi tuna nafasi mbalimbali za kuishi ushirika mtakatifu kupita mipaka ya mataifa. Mungu ametupatia sisi pumzi na roho yake. Na tunomba, “Ongoza njia zetu katika mwelekeo wa amani.” [V]


1 Mwanzo mwa uchungaji wake, Papa Benedicko wa kumi na sita aliandika, “Watu wote ni wamoja na niwa familia moja.” ( ujumbe wa siku ya amani duniani 2006)
Huko Kolkata, wakristu ni wachache ukilinganisha na madhehebu mengine makubwa ya kihistoria. Huko India mvutano kati ya madhehebu wakati mwingine umesababisha vujo kali. Na tena mapatano ya heshima yametoa picha ya hali ya mwelekeo baina ya madhehebu. Sherehe za utamaduniza kila mmoja zinaheshimiwa na mwingine na hata zinaweza zika ni tukio la kushirikiana.

2 Kijana kutoka Lebanon, baba wa familia, alituandikia sisi wakati milibuko mikubwa ilikuwa imepamba moto pande zote za mashariki ya kati. “Kupata amani ya moyo kunawezakana! Wakati ukiwa umefedheheshwa, ushawishi ni kutaka kurudisha kisasi cha kufedheheshwa. Ijapokuwa unahangaika, ijapokuwa chuki inkuwa kwa nguvu sana, ijapokuwa matamanio ya kulipiza kisasi yanakuwa ndani mwetu kipindi tumepungukiwa nguvu(dhoofika). Naamini katika amani. Ndiyo lete amani hapa sasa.!”

3 Baadhi ya mabruda wa Taizé wameishi miaka thelathini Bangladesh, pamoja na watu karibu wote ni waislamu. Wameshiriki maisha ya kila siku na masikini wa kutupwa na waliotengwa. Mmoja wao akaandika, ”Tunavumbua zaidi kushinda wale waliokataliwa na jamii kwasababu ya udhaifu wao na kuonekana wasiofaa mbele ya Mungu.Kama sisi tutwakaribisha wao, watatuongoza sisi tartibu kuachana na dunia yenye mashindano makubwa na kutuongoza kuelekea dunia ya ushirika mtakatifu wa moyo. Katika tofauti kubwa ya madhehebu na tamaduni, uwepo wetu Bangladesh tunataka iwe ni ishara kwamba huduma isio salama ya mabruda na watawa wa kike (masista) kufungua njia ya amani na umoja.”
Kwa kazi aliyoianzisha Mama Teresa huko Kolkata inaendelea kuangaza mbele kwa mbele kupitia kwa masista wake. Kuwahudumia masikini wa kutupwa na kuwaonyesha upendo kwao imedhirisha upendo wa Mungu. Hivyo watu wengi kutoka pande zote za dunia wamekuwa wakitembea katika njia hiyo ya umoja; Bila wao wapi wangekuwa katika ulimwengu huu?.

4 Kutokuwa sawa (tofaauti) ipo siku itapelekea machafuko .Asilimia ishirini (20%) ya idadi ya watu duniani waishiop nchi zilizoendelea, wanatumia asilimia themaniani (80%) ya maliasili ya sayari yetu. Jukumu la kusimamia vyanzo vya nishati na maji ya kunywa yankuwa ni ya umuhimu zaidi na zaidi.

5 Katika tukio la mazishi ya Bruda Roger, mkuu wa nyumba ya watawa wa Grande Chartreuse, Marcellin Theeuwes,aliandika: ?Mfulilizo wa matukio ya hali ya kifo cha Bruda Roger yameambatanishwa kwa nje ambapo kunaleta mwanga kwa huduma sizo salama ambazo aliziendeleza kama njia Mungu anaipedelea ili tuje na kukaa naye.? (Tazama 2 Wakorintho 12:10.)

6 Wakristu wa karne ya arobaini walidhihirisha vema jinsi gani sala na kujitolea nafsi hukamilishana.Kwa yeye kukaa ndani ya ekaristi inatuhimiza kuungana na masikini.Je, unataka kuheshimu mwili wa mkombozi? Ni yule yule aliyesema huu ni mwili wangu, pia akasema:Uliniona nilikuwa na njaa na haukunipatia kitu cha kula.Pale ambapo hukuwatendea moja ya masikini hawa , umenikataa mimi.Hivyo kumheshimu Kristu ni kwa kushirikiana mali (tawala ) zako pamoja na masikini.? (Saint John Chrysostom, Homily 50 on Matthew.)

7 Tayari wakristu wa kizazi cha mwanzo waliamini ya kuwa:Kristu ameshavuja ukuta uliokuwa unawatenganisha watu kwa kutoa maisha yake kwenye msalaba. (Tazama Waefeso2:14-16.)

8 Mkristu aliyewahi kuishi huko Palestina karne ya sitini aliandika ya kuwa: “Fikiria kwamba dunia ni mviringo,kwamba mungu yupo katikati, na kwamba kipenya cha mduara ni njia mbalimbali ambazo binadamu anaishi. Wakati wale wote wanaotaka kuwa karibu na mungu wanatembea kuelekea katikati mwa duara, wanajikusanya pamoja kwa muda sawa kwa Mungu. Kwa kadiri wanavyokaribia kwa Mungu, ndivyo wanvyojikusanya pamoja.Na kadiri wanavyojikusanya kwa pamoja,ndivyo wanavyomkaribia Mungu.” (Dorotheus waGaza, maelekezo ya VI.)

9 “Uhusiano wa kanisa pamoja na madhehebu mengine yanaongozwa na heshima mbili: Heshima kwa binadamu ni katika kutafuta majibu ya maswali ya ndani kabisa ya maisha yao, Heshima ya kutenda ya roho ya binadamu.(,,,) Sala kamili inachochewa na roho mtakatifu, ambaye hupatikana kimiujiza ndani mwa moyo mwa kila binadamu.” (John Paul II, Redemptoris missio).
Hivyo wakristu ,hatuwezi kuficha kuwa katika wa imani yetu ni Yesu Kristu, ambaye anatuhusisha sisi kwa Mungu katika njia nzuri. (Tazama 1 Timoteo 2:5). Lakini mbali na kufanya mdahalo wa kweli haiwezekani, kujitenga kutoka kwake ,sababu Yesu ni wa pekee,ni kwa unyenyekevu wake, hatutaweza kutazama chini kwa wengine kwa jina lake, lakini ni kwa kuwakaribisha wao tu na kuruhusu sisi wenyewe kukaribishwa nao.

10 Mmoja wapo ambaye anaweza kutuunga mkono sisi katika njia hii ni Dietrich Bonhoeffer. Katika masaa yenye giza nene ya karne ya ishirini, alijitolea maisha yake ya mateso ya kishhidi mpaka mwisho (mfiadini).Miezi michache kabla ya kifo chake ,akiwa gerezani aliandika yafuatayo ambayo kwa sasa tunayaimba huko Taizé:
“Mungu ruhusu mawazo yangu yajikusanye kwako.
Kwako kuna mwangaza,usinisahau mimi.
Kwako kuna msaada, kwako kuna ustahamilivu.
Mimi sielewi njia zako,
Lakini wewe wajua njia yangu.”

[IMatthew 25:40.

[IIIsaiah 43:1-4

[IIIBrother Roger, Letter to the People of God, 1976.

[IVSee Luke 13:18-21.

[VSee Luke 1:79.

Printed from: https://www.taize.fr/sw_article4789.html - 6 October 2024
Copyright © 2024 - Ateliers et Presses de Taizé, Taizé Community, 71250 France