To begin the prayer, choose one or two songs of praise.
Zaburi
esu alisali sala hizi za zamani za watu wake. Mara zote wakristu wamepata uzima kwa sala hizo. Zaburi hutuweka katika ushirika wa hali ya juu na waamini wote. Furaha na huzuni zetu, imani yetu kwa mwenyezi Mungu, uhitaji wetu na shauku zetu hutimia katika zaburi.
Mtu mmoja au wawili wanaweza kupokezana wakati wa kusoma au kuimba zaburi. Kila baada ya kifungu, wote huitikia Alleluya au kiitikio kingine. Kama kifungu kinaimbwa kinatakiwa kiwe kifupi, mara nyingi si zaidi ya mistari miwili. Wakati mwingine, waumini wanaweza kuimba kiitikio kwa sauti za chini sana hali mashairi yanaimbwa na waongozaji. Kama mashairi yanasomwa na sio kuimbwa, yanaweza kufanywa marefu. Si lazima sana kusoma zaburi yote mpaka mwisho. Usisite kuchagua vifungu vichache, na mara nyingi vile ambavyo ni virahisi kupatikana.
Masomo
Kusoma maandiko ni njia ya kuzama “ndani ya chemichemi/kisima kisichokauka kamwe ambapo Mungu hujitoa mwenyewe kwa wale wamtafutao” (‘Origen’, karne ya tatu). Biblia ni “barua ya Mungu kwa viumbe wake” inayoviwezesha “kugundua Moyo wa Mungu ndani ya maneno yake” (Gregory the Great, karne ya sita).
Jumuiya zinazosali mara kwa mara huwa na utaratibu wa kusoma andiko la biblia katika mpangilio maalumu. Ila kwa sala za juma au mwezi, somo linalopatikana kirahisi ndilo lichaguliwe, na haswa lile linaloendana na dhumuni/nia ya sala au kipindi hicho. Kila somo laweza kuanza kwa kusema “somo kutoka...” au “injili kama ilivyo andikwa na mtakatifu…” kama kuna masomo mawili, moja laweza kuchaguliwa kutoka agano la kale, waraka, matendo ya mitume au kitabu cha ufunuo; somo la pili ni muhimu litoke kwenye injili mojawapo. Na kwa namna hii wimbo wa tafakari waweza kuimbwa kati ya somo na somo.
Kabla au baada ya somo, ni vizuri kuchagua wimbo unao shangilia mwanga wa kristu. Wakati wimbo huu unaimbwa, watoto au vijana wadogo wanaweza kupita mbele na mishumaa kuwasha taa ya mafuta iliyowekwa juu ya stendi. Ishara hii inatukumbusha kuwa hata kama ni usiku wa giza nene iwe maisha yetu wenyewe au maisha ya kiutu, pendo la kristu ni moto usiotoweka kamwe.
Nyimbo
Kimya
Tunapojaribu kuonyesha ushirika na Mungu kwa maneno, mawazo yetu hayaelewi. Lakini ndani ya nafsi zetu, kwa njia ya roho mtakatifu, kristu anasali kuliko tunavyoweza kudhania.
Ingawa Mungu hakomi kujaribu kuwasiliana nasi, kamwe hii haimaanishi tukome kusali. Sauti ya Mungu mara kwa mara husikika katika sauti za chini sana (minongono) katika hali ya ukimya na utulivu. Kukaa kimya ndani ya uwepo wa Mungu, na ukiwa umemruhusu roho mtakatifu kutawala ndani yako, tayari ni sala tosha.
Kuwaza sana na kwa namna yoyote kufuata misingi fulani ambayo ndani yake hamna kitu, siyo namna ya kupata utulivu wa ndani. Badala yake, kama tungemruhusu Yesu kusali kimya ndani yetu, kama ilivyo imani ya watoto wadogo, siku moja tungegundua kuwa ndani yetu hatuko watupu.
Wakati wa kusali na wengine, ni vizuri kuwa na muda mrefu wa kutosha wa kimya (dk 5-10) kuliko kuwa na vipindi vingi vifupi vifupi vya ukimya. Kama hao wanaosali hawajazoea ukimya, itakua vizuri kuwaelezea kabla maana ya kimya hicho. Au, baada tu ya wimbo kuendelea na kimya, wakati mwingine mtu mmoja anaweza kusema, “Sasa tunaendelea na sala kwa kukaa kimya kidogo”.
Litania ya kusifu
Sala ambayo inatawaliwa na sala fupi fupi au mapambio, ambayo yanafanywa kwa kuimbwa kwa sauti za chini, na kufuatiwa na kuimbwa kwa sauti kubwa na waumini wote, inaweza kufanya “muhimili” ndani kabisa ya sala. Ni vizuri pia kuwaombea wengine haswa familia yote; tunakabidhi yote kwa Mungu furaha na matumaini, majuto na masumbuko ya watu wote, na hasa zaidi wale waliosahauliwa. Sala ya kusifu inatuwezesha kumsheherekea Mungu wetu.
Mtu mmoja au wawili wanaweza kuchukua nafasi ya kuelezea sala fupi au pambio, ambayo hufuatiwa na kiitikio kama Bwana utuhurumie, au sifa kwako ee Bwana. Baada ya sala fupi iliyoandikwa au pambio kuisha, muda unaweza kutengwa ili kuwaruhusu watu kutoa maombi yao wenyewe hasa yale yanayogusa mioyo yao. Maombi haya ni vizuri yakiwa mafupi na kuelekezwa mbele za Mungu; isije ikawa ni nafasi ya watu kuelezea matatizo yao kwa wenzao wakijidai kuwa wanasali. Kila baada ya ombi ni vizuri kuitikiwa na watu wote kwa kiitikio kilekile.
Baba yetu
Sala ya kufunga
Nyimbo
Mwisho, wimbo unaweza kuendelezwa kwa muda. Kikundi kidogo chaweza kubaki kuendelea kuimba kwa ajili ya wale wanaopenda kuendelea kusali.
Watu wengine wanaweza kualikwa kwa ajili ya vikundi vya majadiliano sehemu ya jirani, kwa mfano ili kutafakari kwa pamoja kifungu cha biblia, labda kwa kutumia “johannine hours”. Kila mwezi katika barua za Taizé “johannine hours” zinapendekezwa, mwisho muda kidogo wa kimya nakushirikishana kuhusiana na andiko.
“Vitabu vya nyimbo, nk.
Taarifa za vitabu vya nyimbo na vyanzo vingine vyaweza kupatikana kwenye “vitabu, CD na kaseti za video” sehemu”