Zaidi ya vijana 150 kutoka Kenya, Uganda, Tanzania, Rwanda, Burundi na Jamhuri ya domokrasia ya Congo walihudhuria mafungo yaliyoandaliwa na Mabruda wa Taizé Brothers huko Mji wa furaha – Nairobi wakati wa juma la pili na tatu la mwezi wa nane.
Kiini cha mikutano ilikuwa sala mara tatu kila siku.
Programu ya asubuhi ilihusisha tafakari ya Bibilia iliyoongozwa na mmoja wa mabruda, tafakari binafsi kwa ukimya, na kushirikishana kwenye vikundi vidogo.
Wakati wa mchana, warsha na kutembelea sehemu ya matumaini imetoa namna ya kukoleza mahusiano kati ya imani na maisha. Miongoni mwa sehemu hizo ni:Boma Rescue Centre; mradi wa kurekebishia watoto wa mtaani huko dampo la Mukuru, Maktaba ya Mtakatifu Yohane(St John’s Library) huko Korogocho; lengo kusaidia wanafunzi kazi zao za nyumbani, nyumba ya wasiojiweza (home for the disabled) inayosimamiwa na wamisionari wa Mama Teresa, Nyumba ya wazee; inayosimamiwa na Dada wadogo masikini.
Warsha za mchana pia zilihusisha: haki za binadamu, haki na injili; iliyotolewa na Ann Power, jaji katika mahakama za ulaya kwaajili haki za binadamu huko Strasburg; changamoto za kimazingira,dharura na uwezekano wa utatuzi; iliyotolewa na David Williamson, mtafiti katika kituo cha kidunia cha kilimo na misitu(World Agroforestry Centre) huko Nairobi, mtaalamu wa sayansi ya hali wa hewa; John Ndanbuki ambaye ni fundi seremala huko Kariobangi anajihusisha na majukumu ya taaluma yake na maisha ya familia,pia najihusisha na uongozi wa kanisa na jamii.
Mafungo mengine ya kimataifa ambayo yatayarishwa na mabruda yatafanyika huko Mji wa furaha – Nairobi, kutoka 1 - 5 na kutoka 8 - 12 Desemba 2010.
Kila mwisho mwa Ijumaa na Jumamosi ya mwezi,Mabruda wanaalika vijana kwaajili ya mafungo mafupi huko Mji wa furaha.
Kwa taarifa zaidi wasiliana: Bruda Luc, simu: +254 (0)724 664 198.