Programu za mafungo kila mwezi
Kuanzia ijumaa ya mwisho wa mwezi
Saa 11: Jioni ukaribisho
Saa 1 usiku: Chakula cha jioni
Saa 2:30 usiku: Sala ya jioni na sala kuzunguka msalaba
Usiku katika mabweni ya Mji.
Jumamosi
Saa 1 asubuhi: Sala ya asubuhi, kifungua kinywa.
Saa 2:45 asubuhi: Utangulizi wa Biblia
Tafakari binafsi, kushirikishana katika vikundi vidogo vidogo
Saa 6:30 alasiri: Sala ya mchana
Chakula cha mchana na kuondoka
Mikutano ya kimataifa - Mafungo
April 6 – 10 and 13 – 17
Furaha iliyokaa ndani, acha masikitikao nyuma!
Kumfuata Yesu katika hashiki yake na ufufuko.
Agosti 3 – 7 and 10 – 14
Njia ya furaha, katika hatua za Yesu.
Kristu anabadili maisha yetu na kutufanya mwanga wa ulimwengu.
Disemba 7 – 11 and 14 – 18
Kuamini katika msamaha kunatufanya huru.
Kupokea na kushirikishana ujio wa Mungu duniani.
Kila siku, bruda wa Taizé atatoa utangulizi wa tafakari ya Biblia, ikifuatiwa na muda wa ukimya na kushirikishana katika vikundi vidogo vidogo. Mchana, kutakuwa na kazi na warsha ambazo zitatusaidia kuelewa kiundani zaidi uhusiano wa imani na maisha. Kuishi maisha marahisi na wengine kunatukumbusha kuwa maisha ya kila siku ni sehemu ambapo Kristu anatukusubiria.
Ratiba
Jumatano
Kuwasili kabla ya saa 11
Saa 1 usiku: Chakula cha jioni
Saa 2:30 usiku: Sala ya jioni
Alhamisi, Ijumaa na Jumamosi
Saa 1 asubuhi: Sala ya Asubuhi kisha kifungua kinywa
Saa 3:30 asubuhi: Utangulizi wa Biblia, tafakari binafsi, kushirikishana katika vikundi vidogo vidogo
Saa 6:30 alhasiri: Sala ya mchana, baadaye Chakula cha mchana
Saa 9 mchana: Mikutano, ziara za sehemu za matumaini au warsha
Saa 1 usiku: Chakula cha jioni
Saa 2:30 usiku: Sala ya jioni ikifuatiwa na usiku wa ukimya
Ijumaa jioni sala inafuatiwa na ibada kuzunguka msalaba.
Kusherekea mwanga wakati wa sala ya Jumamosi jioni
Jumapili
Kushiriki ibada katika jumuiya mbali mbali za karibu.
Kuondoka baada ya chakula cha mchana siku ya Jumapili.
Mahali: Malazi rahisi katika domitori na chakula vitapatikana Mji wa Furaha.
Tafadhari njoo na: Biblia, karatasi na kalamu, mashuka, taulo, kandambili, sabuni, ving’arishio viatu, mswaki na vitu vya binafsi.
Gharama ya kushiriki: Kwa siku zote nne za mikutano, 350 KSH, chakula na malazi vikiwemo. Mikutano haipokei misahada toka sehemu nyingine ila inategemea michango toka kwa washiriki.
Kusajiri: Wiki tatu kabla ya mafungo. Tafadhari leta Mji wa Furaha au tuma fomu yako ikiwa imesainiwa na kugongwa muhuli na paroko wako au padri wa vijana, ikiambatanishwa na 150 TSH kwa kila mshiriki. Tafadhali leta kiasi kilichobaki 200 TSH siku ya kuwasili.
Fedha zaweza pia kutumwa kupitia Mpesa: 0724 664 198. Tafahali tambua kuwa idadi ya washiriki si zaidi ya mia moja. Hivyo hatutasa sajiri vikundi vikubwa zaidi ya 10.
Umri: Miaka 18 hadi 30
Tambua ya kuwa kushiriki katika mafungo kunahitaji hali ya utu uzima na kuwajibika, msukumo binafsi wa kushiriki katika programu, kuwa tayari kuchukua sehemu ya kazi, na kutopanga kufanya vitu binafsi tofauti na mafungo n.k.
Jumuiya ya Taizé
Mji wa Furaha
Ng’ambo ya Barabara ya Thika (Geti moja na Redio Waumini, inatazamana na Hoteli ya Safari Park).
PO Box 65171
0618 Ruaraka, Nairobi.
Simu:Br Luc: 0724 664 198, Br. Kombo: 0714 882 753