TAIZÉ

Kigali

Safari ya Imani Duniani

 

Kuanzia tarehe 14 hadi 18 Novemba 2012, kutakuwa na mkutano wa kimataifa wa vijana mjini Kigali: hatua mojawapo ya safari ya imani duniani iliyoanzishwa na mwanzilishi wa Jumuiya ya Taizé hayati Bruda Roger.

JPEG - 29.1 kb
Prayer during the pilgrimage of trust in Nairobi (2008)

Hatua za hivi karibuni katika safari hii ya imani zilikuwa barani Asia (Manila, 2010), Amerika ya Kusini (mjini Santiago Chile, 2010) na Ulaya (Rotterdam,2010). Maelfu ya vijana watakusanyika kutoka Rwanda na nchi nyingine za Afrika Mashariki. Kutakuwa na wawakilishi kutoka Afrika ya Kusini, Madagascar, Sudan, Zambia, Malawi, Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo... na kutoka Ulaya, Amerika na Asia.

Nia ya mkutano ni kumsherekea Kristu, kwa pamoja kwenda katika vyanzo vya imani na kuweza kupata nguvu za kuweka upya nia zetu kwa Kanisa na jamii. Sala ya pamoja (ukimya na nyimbo za tafakari), tafakari ya Biblia, kushirikishana maisha yetu, ukarimu katika familia na jumuia za wakristu kutakuwa chachu ya mkutano.

Asubuhi ratiba itaandaliwa katika parokia za mji na maeneo ya jirani (sala ya asubuhi, kutembelea na kukutana na “watu wa matumaini”). Mchani ratiba itajumuisha tafakari ya Biblia, kushirikishana katika vikundi vidogo vidogo, warsha katika dhima mbali mbali (mambo ya kijamii, maonyesho ya kitamaduni...). Washiriki watapata malazi kutoka kwa familia za Kanisa mahalia.

Ilirekebishwa mara ya mwisho: 22 June 2011