Kushiriki katika mkutano mjini Kigali kunamaanisha kupiga hatua mbele kiroho, na kutafuta njia rahisi za kukuza imani na nia zetu. Wakati wa kujiandaa kwenda Kigali, tunaweza:
1. Kusali pamoja kwenye jumuiya au kwenye vikundi vya sala. Kutusaidia kuifanya safari yetu iwe ya kiroho, ikiunganishwa na maisha ya parokia na vikundi vyetu.
2. Tafakari na wengine “Barua toka Chile”, na haswa kwenye dhima zifuatazo: Kuchagua furaha; Njia ya kuelekea furaha ipo kwenye zawadi ya nafsi zetu, kila siku; Kukaribisha na kushirikishana msamaha wa Mungu...
Washiriki wanategemewa kufuata ratiba yote wakati wa siku nne za mkutano. Maandalizi ni muhimu ili safari ya imani ianze nyumbani: kupokelewa kama wageni, kushiriki kikamilifu katika “kupeana zawadi” na kushirikishana tofauti za lugha, tamaduni na madhehebu.
Kama unaishi Rwanda au nchi nyingine za Afrika Mashariki, ulizia katika parokia yako lini mkutano wa maandalizi utafanyika. Wakati wa miezi ijayo, mabruda wa Taizé na vijana wanaojitolea watafanikisha mikutano hiyo.
Kama unaishi Ulaya, ni vyema kabla ya mkutano wa Kigali kuja Taizé, na kushiriki katika maandalizi ya mkutano.