Tarehe: Kuwasili, kukaribishwa na sala ya kwanza tarehe 14 Novemba 2012, kuondoka Novemba 18 2012.
Washiriki wenye umri wa kuanzia miaka 18 hadi 30.
Malazi yatatolewa na familia wenyeji, (katika kumbi za mashule/vyuo kama itakuwa muhimu).
Vyakula vya kawaida vitatolewa: kifungua kinywa sehemu ya malazi; chakula cha mchana na cha jioni mahali pa mkutano pamoja baada ya sala za mchana na za jioni.
Ratiba ya Mkutano
Jumatano 14.11.2012
Kukaribiswa kati ya saa 1 asubuhi na 6 mchana na usafiri kwenda parokia wenyeji
Saa 10 jioni kuondoka kwenye parokia
Saa 11:30 Jioni: Chakula cha jioni na Sala ya pamoja
Saa 1:45 Usiku: usafiri kurudi kwenye parokia na familia wenyeji
Alhamis 15.11.2012, Ijumaa 16.11.2012, Jumamosi 17.11.2012
Saa 2:00 asubuhi: Sala ya asubuhi kwenye parokia, ikifuatiwa na ratiba ya asubuhi parokiani: "Kutembelea na mikutano na watu wa matumaini katika jamii yetu"
Saa 5:00 asubuhi: Kutoka kwenye parokia
Saa 6:00 mchana: chakula cha mchana na Sala ya Pamoja ikiwa na masomo mafubi ya Biblia, nyimbo za tafakari na ukimya
Mchana: Tafakari ya Biblia, kushirikishana katika makundi madogo madogo kwenye dhima mbali mbali (mambo ya kijamii, maonyesho ya tamaduni…)
Saa 11:30 jioni: chakula cha jioni na Sala ya Pamoja
Saa 1:45 Usiku: usafiri kurudi kwenye parokia wenyeji na familia
Jumapili 18.11.2012
Ibada katika parokia walezi
Kuondoka
Taarifa kwa:
vijana waishio Rwanda
vijana waishio nchi nyingine za Afrika
vijana waishio nje ya Afrika