Ili kusaidia kufanikisha mkutano huu, itakuwa vyema kujitoa kabla na kuheshimu kuingia kwenye mtindo wa maisha ya wenyeji wetu.
Kuongeza wigo wa sala zetu na kumuomba Mungu kututayarisha ili kutambua hazina za ubinadamu zilizopo hata katikati ya vipindi vigumu ni njia muhimu ya kuanza maandalizi.
Pasi ya kusafiria na visa:
Kutegemeana na utaifa wako, ni muhimu kupata visa au makubaliano ya kuipata wakati wa kuwasili kabla ya kuanza safari. Maelezo zaidi yanaweza kupatikana hapa:
http://www.migration.gov.rw/
Kuchangia Gharama:
Wale waishio nje ya Rwanda, tafadhali wawasilane na Taizé kufahamu kiasi cha mchago.
Safari:
Tafadhali tutumie taarifa za safari yako.
Mwisho wa kujiandikisha:
1 Octoba, 2012 kupitia parokia yako au mlezi wa vijana
Hifadhi tangazo: