TAIZÉ

Hija ya imani itakayofanyika Nairobi, Kenya

 
Wakati wa mkutano Geneva, Bruda Alois alitangaza, “Tutaendeleza mikutano ya vijana katika mabara mengine. Baada ya Asia na Amerika ya kusini (Latin America), Mwaka ujao Tutaenda Afrika. Kuanzia tar 26-30 Novemba tutakaribishwa ukanda wa chini ya Ikweta, Afrika Mashariki, nchini Kenya, katika mji wa Nairobi.

Utoaji msaada kwa wakristo Kenya

Kwa kipindi cha muda wa siku chache zilizopita, baadhi ya mabruda wamerudi Nairobi :
17 Februari: “Kidogo kidogo tunafanya tena mawasiliano na mji, jumuiya mbalimbali pia na watu binafsi. Tunaona misururu ya magari barabarani, matatu (mabasi madogo ya abiria) yenye sauti kubwa, msongamano wa watu katikati ya mji, mavumbi…Polepole ,watu wanaanza kutulia baada ya machafuko ambayo yalipamba moto katika baadhi ya maeneo wiki zilizopita. Kila mtu mawazo yake yanalenga matokeo ya majadiliano, baadhi wanajitahidi kutoa misaada ya dharura kwa wale walio hama makazi yao au kusaidia kurudisha hali ya amani ya kawaida… Huu ni wakati mwafaka kwa nchi kwani, kupitia majaribu kama haya, inawezekana kupata ufahamu bayana wa jukumu la kila mtu katika kuleta amani na haki kwenye jamii. Makanisa yanashiriki katika mambo haya yote na husaidia watu kutafakari juu ya yale ambayo nchi imepitia. Bado kuna mengi yanayohitaji kufanyika. Wengi hushawishika kutokana na propaganda. Mitazamo ya wengi bado hutofautiana. Hata hivyo, kwa upande wa majirani, ukisikiliza maongezi yao, wanazungumzia habari za umoja kati ya watu wa makabila tofauti na hata kutoa ushuhuda juu ya upendo na mshikamano uliopo…”

26 hadi 30 Novemba 2008

Kutangazwa kwa mkutano kumekuja wakati mahususi kwa Kenya. Kila siku vyombo vya habari vilitoa habari za vurugu zilizofuatia uchaguzi. Kenya na wahanga wa machafuko yaliyotokea waliwekwa katika sala zilizoendelea katika mkutano wa Geneva.

Mch. Simon Githiora na Pad. Peter Muigai, ambao wanahusika na umoja wa vijana wakikatoliki na wasiowakatoliki Kenya, walikuja Geneva, haswa kwa ajili ya kutangazwa kwa mkutano wa Nairobi. Pia vijana wawili kutoka Kenya, ambao nao walikuja kwa ajili ya mkutano, walizungumza baada ya Bruda Alois:
Japhet: Tuna furahi kutoa mwaliko kwa hatua ya afirika kuwa na “hija ya imani duniani”. Tutawaonyesha jinsi ambavyo vijana wanasaidia kuleta matumaini katika nchi yetu. Mutaona pia jinsi anbavyo, undugu/ukarimu katika familia na jumuia ulivyo muhimu kwetu.
Peter: Tunataka tuwaambie kwa Kiswahili “Karibuni Kenya, Welcom to Kenya!”

Jinsi watu walivyochukulia tukio kwa mara ya kwanza

JPEG - 26 kb

Mkutano ulikaribishwa kwa hamasa kubwa sana.

Kutoka Uganda: Nina furaha kubwa sana kupata habari kuwa, Taize inaandaa mkutano Nairobi. … Kwangu mimi, mkutano huu umekuja kwa wakati, kwani Vijana wengi wa Africa wanahitaji maisha rahisi kiroho, Kama ambavyo Kenya na nchi nyingi za kiafrika zinapitia misukosuko ya kivita na fujo wakati wa uchaguzi, ukosefu wa elimu… Niko tayari kutoa msaada na usharuri wa aina yoyote ulioko ndani ya uwezo wangu, katika maandalizi ya mkutano huu wa vijana. Robert.

Kutoka Tanzania: Kwa wale tuliowahi kufika Taize, tutajaribu kualika vijana wengine toka Tanzania washiriki katika mkutano wa Nairobi. … Tumeamua kukutana kila Jumapili ya kwanza ya mwezi, kwa ajili ya sala, kuimba, kushirikishana na kufanya tafakari, kwa sasa twaweza kuanza kujadili ni jinsi gaini tutashiriki katika maandalizi ya mkutano wa Nairobi. Caroline.

Kutoka Uganda: Hatimaye, Taize inaandaa mkutano wa Afrika Mashariki. Hii inastaajabisha sana na natumaini kuwa vijana watapenda na wataweza kushiriki, pia wamefahamishwa kwa wakati! Nitatoa msaada wangu kadiri nitakavyoweza pia nitawaombea….

Kutoka Uganda: Tunayo furaha kubwa sana kusikia kuwa, mkutano wa Kiafrika unaandaliwa, na zaidi kwa jinsi ambavyo utakuwa wa kwanza kwa aina yake kuandaliwa baada ya miaka mingi. Hapa Uganda … daima tunawasiliana baina yetu na tuna matumaini ya kuwa sehemu ya mkutano wa Nairobi. Isaiah

Kutoka Uganda: Kwa kiasi fulani tumezidiwa na mambo kwa hizi siku chache baada ya matukio yaliyotokea Kenya kufuatia uchaguzi wa Raisi na wabunge tar. 27 Desemba. Kwa kuona jinsi fujo zimezidishwa na tofauti kati ya Wakenya, naamini kuwa mwaka 2008 ni wakati mwafaka kwa kuandaa mkutano huu ili kujaribu kupatanisha watu na kuwafanya wafikiri kwa pamoja jinsi ya kushinda vikwazo vitutenganishavyo. Ni kwa vipi tunaweza kushinda tofauti kati ya Wakikuyu na Waluos, kati ya Waganda na Wakenya, na kadhalika?
Mimi nafikiri kuwa hapa Kampala, kujiweka tayari kwa ajili ya tukio hili, tungeweza kuunda vikundi vidogo vidogo vya maandalizi, na labda viongoze sala za mara kwa mara Makerere. Tunaweza kuwasiliana na parokia mbalimbali, majimbo na mashirika ili wawakilishi wafanye maandalizi pamoja nasi. Boniface

Mabruda Kenya

JPEG - 22.1 kb

Kwa ajili ya mafanikio ya mkutano wa Afrika Mashariki mwaka huu, mabruda watatu wa jumuiya walitembelea Kenaya mwezi Oktoba 2007, Mmoja wao kutoka Kongo (DRC), anaandika “Tulifika salama na ilikuwa furana kubwa sana, kurudi tena kwa mara nyingine katika baadhi ya sehemu tulizowahi kutembelea katika ujio wetu wa kwaza mwezi Februari! Kwa mara nyingine tuna tumia usafiri wa uma jijini. Mji umechangamka sana! Tunakaa jirani na kuitwako “Ruaraka”, katika kituo cha vijana kitaifa, ambamo kuna kanisa dogo ambapo tunafanya sala za asubuhi kila siku, na wakati mwingine adhimisho la Ekaresti takatifu tukiongozwa na Padre kiongozi wa kituo hicho. Maisha yetu kama kikundi kidogo cha muda cha mabruda watatu, ni ya hali ya kawaida sana. Tuna vitu vichache sana lakini hatuoni kupungukiwa na kitu… Jana tulitembelea bonde la Mathare na Kariobangi. Ilikuwa furaha sana kuona baadhi ya vijana tunaowafahamu, kama vile Ken, Ben na Alicie, ambao walikuwa Taize mwaka huu; na wengine ambao waliwahi kufika miaka ya nyuma. … Kukawa na sala katika Kanisa la Mtakatifu Martin pamoja na watoto thelathini na takribani vijana ishirini. Ilitukumbusha sala za nyumbani mwa mabruda wetu wa Senegal: sala rahisi sana, iliyojaa furaha. …”

JPEG - 21.4 kb

Mmoja wa mabruda wengine anaendelea, “Mwezi huu wa Octoba umewezesha maandalizi ya msingi ya awali kwa ajili ya mkutano wa vijana utakaofanyika mwishoni mwa Novemba, 2008. Tuliweza kutembelea parokia thelathini, shule, jumuiya za kikristu… Kuna mawasiliano mazuri na Waprotestanti, Waanglikana na makanisa ya Kikatoliki. Pia mawasiliano yameanza kwa makanisa ya (Kibaptist na Copt)… Kuanzia mwezi wa pili mwakani, tutaweza kutembelea na kufanya mawasiliano na vijana… Changamoto zinatofautiana: kuweka mambo sawa, kuanzisha tafakari na zaidi sala katika ukimya … makaribisho ya wenyeji; kushiriki kwa vijana kutoka makundi mbalimbli na jamii tofauti… Mkutano kuwa na dhana ya kimataifa; ugeni wa jambo; maombi ya msaada katika maandalizi ya siku hizi; hitaji la sala katika mkutano– haya yote yanaonyesha njia mbalimbali za kuwahamasisha vijana...

Mabruda wa kwanza watawasili Nairobi katikati ya mwezi wa pili.

JPEG - 22.5 kb
Ilirekebishwa mara ya mwisho: 10 November 2008