TAIZÉ

Nairobi

Tafakari na Bruda Alois

 
Mkutano wa Nairobi ulifanyika kuanzia tarehe 26 hadi 30 Novemba 2008
Kila jioni ya mkutano, Bruda Alois alitoa tafakari
Tafakari hizo zimeandikwa hapa.

Alhamisi 27 Novemba

Ni furaha kubwa sana kujumuika nanyi hapa Nairobi.Tuko hapa pamoja kujiuliza swali:Je ni yapi yametuleta kujumuika na wengine leo?

Kwa miezi kadhaa, zaidi ya parokia sabini zimefanya kazi kwa pamoja kufanikisha makaribisho haya.Tungependa kutoa shukrani kwa wote ambao wamejitolea kuwezesha kuwepo kwa mkutano huu.

Kuna mengi kati yetu,mmetoka katika nchi mbalimbali katika bara la Afrika; na wengine mmetoka mabara mengine kote ulimwenguni. Huu umoja ni jambo ambalo tungependa kulizawadia na kulihimiza. Sote tuko katika jumuia moja yaani kanisa , kwani sote tu watoto wa Mungu.

Kwa upande wangu ni furaha iliyoje hasa kuwa katika mji huu tena. Miaka thelathini iliyopita, nilikuwa hapa Nairobi kwa majuma kadhaa na Brother Roger, mwanzilishi wa shirika letu pamoja na wengine. Tuliishi tukiwa majirani na kitongoji duni cha Mathare Valley.

Nakumbuka hizo siku sana. Tulikaribishwa na watoto na walikuwa wakijumuika nasi katika maombi na kutufunza wimbo ¨Simama¨. Walitusaidia sana kutafuta urafiki na uaminifu. Wakati huo wengine wetu waliishi Mathare Valley na Kangemi kwa miaka kumi.

Leo duniani kote, jamii na maisha ya kila mmoja yanabadilika haraka sana. Kumekuwa na maendeleo mengi duniani, lakini umaskini na ukosefu wa haki bado unaendelea, kuna unyonge na kushtumiwa kuhusu maisha ya baadaye ambazo zinaendelea kupamba moto.

Kuimarika kwa uchumi kunafaa kuambatana na maisha ya kila mmoja ili kuleta uwiano maishani. Katika udumishaji na kuchanganyikiwa kwa hisia za watu, tukiwa hapa Nairobi naomba tujiulize swali hili, Ni maisha yapi ambayo tunaishi? Tutapata mwelekeo wapi?

Karne nyingi kabla ya Yesu kuzaliwa Nabii Isaya aliangazia kisima hiki aliposema ¨lakini wote wanaomtumania Mwenyezi-Mungu. Watapata nguvu mpya. Watapanda juu kwa mabawa kama tai; Watakimbia bila kuchoka watatembea bila kulegea¨ (Isaya 40.31)

Tunawezaje kukifungua kisima hiki kama si kukubali uwepo wa Mungu? Kwa kufanya hivyo, tunakaribisha mwelekeo na furaha ya Bwana. Kwa kufungulia Mungu milango ya nyoyo zetu, tunamtengenezea njia ili aweze kuzuru wenzetu pia.

Mungu yuko katika maisha ya kila mmoja wetu; awe ana imani au hana. Katika mwanzo, Bibilia imeelezea vizuri sana jinsi Mungu aliweka Roho Mtakatifu katika maisha ya binadamu. Roho Mtakatifu anatuinua, kututembeza na kutengeneza maisha yetu.

Wakati Yesu alikuja duniani siku ya krismasi, alituelezea kuhusu mapenzi ya Mungu yasiyo na kifani. Na kwa kujitolea hadi mwisho, alionyesha uwezo wa Mungu ndani ya maisha ya binadamu. Tangu kufufuka kwa Yesu, hatuwezi kuteseka tena.

Tangu nyakati hizo za Pumzi ya Bwana, Roho Mtakatifu amekuwa nasi mpaka leo. Kupitia kwa Roho Mtakatifu, Mungu amekubali jinsi ulivyo hata kama hujiamini. Hatuwezi kuchoka tunaposikiza maneno ya Nabii Isaya. ¨Mungu atakupa upendo wake, na dunia itakuwa na mazao mazuri¨

Tifurahie jinsi tulivyoumbwa, tusijidunishe. Tujaribu kujiinua hata kama si kwa ukamilifu. Hata kama tunafinyika hapa duniani, tukubali maisha yetu ni zawadi, kila siku Mungu anatupa uwezo mpya.

Hapa Bara Afrika, watu hupitia majaribu ya kudunisha hadhi yao. Majaribu na ugumu haufanyi tukose furaha, hata katika ugumu tunafaa kumshangilia Bwana. Wengi hujipa tumaini maishani. Mara kwa mara, wanawake huwa mbele hasa kwa kufanya kazi katika familia na jamii kwa ubunifu na uvumilivu.

Tukiwa kwa shida hasa umaskini, ukosefu wa haki au vitisho maishani, tunafaa kufanya nini ili tuwe na tumaini? Ni mipango gani tuko nayo karibu? Tunafaa kuendea wengine kwa uwazi kwa njia rahisi? Vukeni mipaka! Tuwasaidie wanaoteseka! Tuwatembelee wanyonge na wanaoteshwa!

Popote ulipo, tuonyeshe ishara ya mapenzi pekee yako na kwa wenzako hasa wakati wa shida; Kwa njia hii tunaweza kungundua uwepo wa Kristo hata pale hatumtarajii. Amefufuka kutoka kwa wafu, Yuko hapa katika maisha yako. Yuko mbele yetu kutuongoza na kwa kupitia Roho Mtakatifu, ataibadilisha sura ya dunia.

Ijumaa tarehe 28 Novemba

Jana nilizungumzia kuhusu umuhimu wa uwepo wa Mungu katika maisha yetu. Hapo ndipo tunapata tumaini la kujadiliana .Ili kutaka kujua uzuri wa uwepo wa Mungu, unafaa kujiuliza,Je unajua thamani ya Bibilia katika maisha yetu?

Nilikuwa mji wa Rome majuma matatu yaliyopita.Nilikaribishwa kwa warsha iliyowaleta Bishops kutoka ulimwengu wote pamoja.Huko nilikutana na Cardinal Njue, alikuwepo.Mada ya warsha ilikuwa Bibilia, neno la Mungu na nafasi yake katika maisha yetu.Tulisikia ushuhuda kutoka kote duniani.Ushuhuda mwingi ulitusisimua kama madini yenye thamani na nitatoa mifano miwili.

Bishop mmoja kutoka Ufilipino, Bara Asia alizungumzia jinsi ya kuwa msikivu.Alisema ili kulielewa neno la Mungu vizuri, tunafaa kuwa wasikivu. Kwanza:Alizungumzia matokeo ya kutosikiliza neno la Mungu kama vile migogoro katika jamii, tofauti kubwa kati ya vizazi na nchi, shutuma…..Alisema kanisa linaweza kuleta uwiano kupitia kujadiliana.

Kisha akasema maneno yenye uzito sana.Mungu anazungumza, lakini hazungumzi tu, Mungu pia husikiliza.Hasa husikiliza wajane, mayatima,waliohukumiwa na wanyonge wenye sauti zao hazisikiki.Ili kuelewa neno la Mungu, tunafaa kujifunza kusikiliza jinsi Mungu hutusikiliza.

Bishop mwengine kutoka Latvia, nchi ndogo kaskazini mwa Bara Uropa alitoa ushuhuda wa kusisimua.Alisema katika nchi yao, wakati wa utawala wa kikomunisti wa Soviet ambao uliisha miaka ishirini iliyopita, watumishi na waumini waliuawa kwa kutangaza neno la Mungu tu.Mtumishi aitwaye Victor kutoka Latvia alishikwa kwa kumiliki Bibilia. Askari walitupa Bibilia sakafuni na kumwamuru aikanyagie chini.Lakini alipiga magoti na kuibusu Bibilia.Kwa kufanya hivyo, alihukumiwa kifungu cha miaka kumi na kazi ngumu gerezani katika mashamba ya barafu huko Siberia.

Tukisikia ushuhuda kama huo, tunaona jinsi Bibilia inapendwa na kugeuza maisha ya watu wengi duniani.Tunashukuru kanisa leo kwa juhudi zake za kugawa na kusambaza Bibilia na neno la Mungu kwa kila mmoja,Ingawa si kila mtu ana Bibilia, njooni pamoja katika parokia tusome na kuelewa umuhimu wa Bibilia maishani mwetu.

Kweli si rahisi kusoma Bibilia.Tunapata vifungu ambavyo hatuvielewi.Tunahitaji usaidizi ili kuelewa tuliyosoma.Ili kurahisisha kuelewa Bibilia, kuna mambo mawili muhimu ya kuzingatia.

Kwanza .sote tukumbuke kiini cha Bibilia katika mapenzi ya Mungu na upendo wa jirani.Kwa Yesu , hii ni jumla ya vifungu vyote katika Bibilia.

Jambo la kutamausha ni kwamba Bibilia imezungumzia hadithi yote ya upendo.Hiki ni chanzo cha upendo wa kwanza, lakini kuna vikwazo na kutoaminiana.Lakini Mungu hachoki kutupenda.Yeye hutufungulia milango,hututafuta.Hata hivyo Bibilia ni hadithi ya uaminifu wa Mungu.Siku ,moja aliwaambia watu wake hivi kupitia kwa nabii mmoja: “Je mwanamke humsahau mwanawe mdogo kweli,,,,, hata kama wanawake husahau,sitawasahau”

Jambo jingine ni,kupitia kwa kuja kwa Kristu,Mungu hushiriki maisha na mateso yetu hadi wakati wa kifo.Kristu amebeba ujumbe maalum kutoka kwa Mungu.Kwa hivyo,Injili inatueleza Kristu mwenyewe ni Neno la Mungu.Tunaposoma Bibilia, tunakutana na Yesu.Ni sauti yake ndiyo tunasikiliza na tunajumuika katika uhusiano Naye.

Hii ndiyo sababu Taizé tunapenda kuimba neno kutoka kwa vitabu kama tunavyofanya tukiomba pamoja.Kurudiarudia kuimba neno la Mungu kunafanya lizame ndani yetu.Tunapenda pia kuwa pamoja kwa kimya kirefu.Kwa kimya, neno la Mungu linaweka mizizi na kukua ndani yetu.

Mara nyingine tunakumbuka neno moja tu.Muhimu ni kuweka haya yote katika matendo.Ni kupitia matendo ndio neno la Mungu linaeleweka.Labda kila mmoja anafaa kujiuliza:Neno gani limegusa nafsi yangu kwa mkutano huu na ninaweza kuliweka katika matendo?

Jumamosi tarehe 29 Novemba

Jioni ya leo ningependa kuchukua fursa hii kuwapongeza kwa moyo wa dhati hasa kwa makaribisho na mapokezi ambayo tumepata hapa Nairobi. Kwa hakika tunatoa shukrani kwa familia, madhehebu/ dini mbalimbali na parokia zote ambazo zimetufungulia milango kutukaribisha kwa nyumba zao.

Mkutano huu wa Nairobi umechangia kujenga uhusiano mwema zaidi na kupuzilia mbali maovu yote ambayo yangesababisha kutoelewana au kutonesha vidonda vya awali. Hatuwezi kubadili yaliyopita, lakini kwa siku hizi, tumekuwa na furaha ya kuvuka mipaka na kupokea kutoka kwa kila mmoja wetu.

Makaribisho ambayo tumepewa na wakristu wa Nairobi yametusaidia kuvumbua jinsi kanisa ni mahali palipo wazi kwa uhusiano wa wote. Kesho tunaenda nyumbani. Tungependa kuzingatia uhusiano huu katika maisha yetu ya kila siku.

Sote tumepewa kipawa cha kuishi katika uhusiano na Kristu. Si kwa kukosa sababu Anapotueleza katika injili, “Siwaiti watumishi tena, bali nawaita marafiki.” Anatuambia sote; tu karibu na Mungu, na litasalia kuwa ukweli kila mara.

Hata kama imani yetu ni ndogo, hata kama tunahisia ya kutoamini, Mungu hachoki kuwa rafiki wetu.

Hapa kuna ujumbe unaofafanua, ni ujumbe wa uhusiano. Umeanza karne ya sita, umetoka kaskazini mwa Afrika, Msiri. Tunamuona Kristu akimwekea rafikiye mkono kwa bega na kutembea naye, ili kuwa naye.

Kila mmoja wetu anafaa kukumbuka sisi ndio huyo rafiki wa Kristu. Hata kama Kristu, alifufuka kwa wafu, haonekani machoni petu, tunafaa kumuachia maisha yetu. Anatembea kando ya kila mwanadamu bila ubaguzi.

Ujumbe huu pekee unafaa kutuunganisha kwa maombi pamoja na Mungu.

Na uhusiano huu na Kristo ni jambo ambalo linaonekana na kujitokeza kati yetu. Kristu hutuunganisha pamoja kwa jumuia moja – kanisa ambayo ni familia ya Mungu. Tuendeleze uhusiano huu na kukemea vizuizi vyote ambavyo vipo.

Katika Afrika, ingawa kuna mambo mengi yanayoligawanya bara, wengi wamekuwa mashujaa wa kutafuta amani na maridhiano.Kwa wakristu, ni hali ya kushikilia tumaini : ubatizo kwa jina la Kristu una nguvu kuliko migawanyiko.Kuna wakristu wengi Afrika ambao maisha yao yametishiwa kwa kushikilia imani.

Wakati tunagundua uhusiano na upendo wa Mungu kwa kila mmoja wetu,tunavumbua ushujaa mpya wa kuongeza uhusiano kwa wale wanyonge hasa wenye tunafaa kulinda.Kanisa la Afrika huwasikiliza sana wanaotupwa na kutengwa.

Uwezo wenu wa kukaribisha na kujitolea kwa haki ni jambo ambalo tungependa kushirikisha watu wa bara lote la Afrika.Mwisho wa mwezi wa Desemba kutakuwa na mkutano mkubwa wa vijana kule Brussels, Ulaya.Baadaye kutakuwa na mkutano mwengine wa vijana Bara Asia,Tutawaletea urafiki na uhusiano wenu.

Tumetengeneza nakala kadhaa za ujumbe wa uhusiano na urafiki kwa kila nchi ya Afrika ambayo imewakilishwa hapa.

Huu ujumbe utakuwezesha kuwapa moyo vijana kuja pamoja kwa mji mmoja au mwingine,parokia moja au nyingine,kwa hospitali au kituo cha kuwaangalia watoto walioachwa au mahali popote watu wanateseka.

Kwa hii njia rahisi, tunaweza kupeleka habari njema za Injili na kuwacha vigezo vya wamishionari katika imani yetu.Kuwepo kwa ujumbe huu utakuwezesha kuunganisha nyoyo za watu.

Leo ni juu yenu, vijana ambao mmeitikia wito wa kutangaza Injili kwa wengine.Kumbuka ; Kristu anatafuta uhusiano wako.Anaweka Roho Mtakatifu ndani yako.Anaenda mbele na kutembea popote uendapo.

Ilirekebishwa mara ya mwisho: 24 December 2008