TAIZÉ

Mikutano Taizé

Mwaka

 

Mikutano ya kimataifa,
Mikutano ya wiki baada ya wiki,
To go to the wellsprings of trust in God and others.

Wiki moja hapa Taizé inaweza kutusaidia kuyatafakari maisha yetu katika mwanga wa injili: kusali pamoja mara tatu kwa siku, kutafakari vyanzo vya imani na kufanya kazi kwa ajili ya wengine

Kila siku mabradha wa jumuiya hutoa somo la biblia kwa ajili ya kutafakari, likifuatiwa na muda wa ukimya na kushirikishana katika makundi madogo madogo

Mchana, kuna warsha zinazosaidia kujenga uhusiano kati ya
maisha ya kiimani na ya kwenye maeneo ya kazi, umoja, maswali ya kimaisha, sanaa na utamaduni katika kutafuta amani ya dunia

Pia kuna muda wa ukimya na kutafakari kwa wiki nzima au mwisho wa wiki, kwa vijana wanaopenda. Hawa, hupata muda wa kumsikiliza na kumtafakari Mungu anapoongea nao katika sala, na kutafakari biblia au kupitia matukio katika maisha yao

Baadhi ya vijana wanatafuta njia za kumfuata Kristu kwa maisha yao yote

Wiki chache kabla ya pasaka, na wakati wa miezi ya kiangazi, tafakari ya pamoja inatolewa kwa watu wenye umri wa kati ya miaka 25 hadi 35.

vijana wanaweza kuishi Taizé kwa wiki kadhaa, wakiwakaribisha wengine wapya na kujijenga wakiongozwa na bradha au sista.

Mikutano ya msimu wa kiangazi huwakutanisha pamoja vijana kati ya elfu nne au tano kutoka zaidi ya nchi 80. Wengi hugundua, pamoja na kwamba wametawanyika duniani kote, wakristu wanaweza kudumisha tumaini kwa wote

Kwa kuzoea maisha ya kushirikiana na wengine, vijana hugundua kuwa maisha yao ya kila siku ni sehemu ambapo upendo wa kristu unaweza kujidhihirisha na pia mahali ambapo maisha tofauti ya baadae yanawezekana.

Ilirekebishwa mara ya mwisho: 14 August 2007