TAIZÉ

Jumuiya

Tangu ujana wangu, Nafikiri sijawahi kupoteza ufahamu kuwa maisha ya jumuiya yanaweza kuwa ishara kwamba Mungu ni upendo, na upendo pekee. Taaratibu, huu msukumo ukawa wazi ndani yangu kuwa ilikuwa ni lazima kuumba jumuiya ya wanaume walioamua kutoa maisha yao yote na ambao watajaribu kuelewana baina yao na kupatanashwa, jumuiya ambayo ukarimu wa moyoni na urahisi vitakuwa katikati ya kilakitu.

Bruda Roger: “Mungu ni upendo pekee”