TAIZÉ

Yohane Paulo II akiwa Taizé

"Muda ule mdogo wa masika!"

 
Papa Yohane Paulo II alitembelea jumuiya ya Taize 5 /10/ 1986. Baada ya muda wa sala na kila mmoja aliye kuwepo Taize, Papa alikutana na Mabruda wa jumuiya.

Wapendwa mabruda, katika mkutano huu wenye uhusiano wa karibu sana kama ule wa kifamilia, napenda kuonyesha furaha yangu ya ndani kabisa na imani niliyonayo kwenu, kwa kutumia haya maneno marahisi kabisa ambayo Papa Yohane XXIII ambaye aliwapenda sana, kwayo, alimsalimia Bruda Roger siku moja: ‘“Ah, Taizé, that little springtime!”’ Ninachokitamani ni hiki, kwamba Bwana Mungu awafanye kuwa kama kipindi cha vuli ambacho huchanua na kuwafanya wanyenyekevu, katika furaha ya injili na upendo wa kindugu usio na kificho.

Kila mmoja wenu alikuja hapa kuishi kwa huruma ya Mwenyezi Mungu na jumuiya ya Mabruda. Kwa kugeuza na kukabidhi maisha yenu yote kwa kristo, na kwa kumpenda, mmeshapata haya yote mawili.

Zaidi ya hapo, ingawa hamkuwa mmetarajia, mmeona vijana wengi sana maelfu kwa maelfu kutoka sehemu zote za dunia wakija kwenu, wakivutiwa na sala na maisha yenu ya jumuiya. Kwa vipi tusifikiri kuwa vijana hawa ni zawadi na njia ambayo Bwana Mungu anawapa shauku ya kuwafanya mzidi kubaki kuwa pamoja, katika furaha na uhalisia wa zawadi yenu, kama wakati wa neema na baraka ‘springtime’ kwa wale ambao wanatafuta maisha ya kweli?

JPEG - 14.5 kb

Katika siku zenu zote, kazi, mapumziko, sala, kila kitu kinafanywa cha kuvutia kwa neno la Mungu ambalo mnaliishi, ambalo linawafanya kuwa wanyenyekevu, kwa maneno mengine watoto wa Baba wa mbinguni, Ndugu na watumishi wa wote katika furaha.

Sisahau kuwa katika mwanzo wa aina yake, na kwa namna Fulani ya wito ambao bado haujakamilishwa, jumuiya yenu inaweza kuamsha hali ya kustaajabisha, kutoeleweka na kutoaminika. Lakini kwa sababu ya nia yenu nzuri ya kuleta maelewano kati ya wakristu katika ushirika kamili, na kwa sababu ya upendo wenu kwa kanisa, mtaweza kuendelea, ninauhakika kuwa kwa mapenzi ya Bwana mko tayari.

Kwa kusikiliza hoja au mapendekezo ya wakristu wa makanisa mbalimbali na jumuiya za kikristu na kuchukua yale ambayo ni mazuri, kwa kubaki katika majadiliano na wote lakini bila kusita kuonyesha matarajio na mipango yenu, hamtawakatisha vijana tamaa, na mtakua vyombo vya kuhakikisha kuwa jitihada zinazohitajika na kristu kurudisha hali ya umoja wa mwili wake unaoonekana katika ushirika wa imani moja isiyo fifia.

Mnajua ni kwa kiasi gani mimi binafsi ninavyochukulia misingi ya muungano wa makanisa, umuhimu wa majukumu niliyonayo na kipaombele cha uchungaji katika usharika wangu, na kwa hiyo naomba sala zenu.

Kwa ninyi wenyewe kutamani kuwa “mfano wa jumuiya ‘parable of community’”, mtawasaidia wote mnaokutana nao kuwa waaminifu katika kushikamana na madhehebu yao, matunda ya elimu zao na chaguo lao katika dhamira zao, lakini pia kuingia zaidi na zaidi ndani kabisa ya imani ya ushirika ambao kwawo kanisa liko katika mpango wa Mungu.

Kwa zawadi yake kwa kanisa, Kristo anatoa kwa kila mkristu msukumo wa upendo na kuwapa moyo mkubwa wa kutengeneza haki na amani, kuweza kuunganisha katika fikira zao jitihada kulingana na injili kwa ajili ya uhuru wa wanadamu, kwa kila mwanadamu, na kwa utu wote.

Wapendwa Mabruda, nawashukuru kwa kunikaribisha na hivyo kunipa nafasi ya kurudi tena Taizé. Bwana awabariki na awape amani na upendo wake!

Ilirekebishwa mara ya mwisho: 14 August 2007

“Mtu hupita Taizé kama yeye apitaye karibu na chemichemi ya maji. Msafiri husimama, akiishaizima kiu yake, huendelea na safari yake”.

Yohane Paulo wa pili