TAIZÉ

Hija ya matumaini duniani

 
JPEG - 30.8 kb

Mwanzo wa yote ni mkutano

Wakati wa mkutano wa Ulaya hapo Zagreb – moja kati ya hatua mpya zilizofikiwa katika hija ya matumaini duniani – familia za Croatia waliwakaribisha nyumbani kwao baadhi ya vijana wa Kiserbia ambao walikuja kwa siku tano za sala na kushirikishana; ikiwa ni muda mfupi sana baada ya kuisha kwa vita iliyowatenganisha watu hawa.

Mara baada ya mkutano wa Lisbon, mmoja wa vijana aliuelezea kama “sherehe ya mataifa” iliyofanyika Desemba 31, “kengele ya usiku wa manane iliposikika, wote walikumbatiana. Walibadilishana salamu na kutakiana kila la kheri. Marafiki wapya walitafutana katika makutano hayo ya watu. Tuliuzunguka moto mkubwa uliowashwa, tukiimba na kupeana shukrani kwa ajili ya mkutano huu, kwa ukaribisho na zawadi ambazo tulibadilishana.

Hija ya matumaini ni ya kwanza kufanyika kwa mkutano wote; tukiwa na Kristu mfufuka na wengine. Asante kwa muda ya sala za pamoja, tunapojitoa kwa Mungu. Kupitia kushirikishana na ukarimu, kila mmoja hukubali kuvishinda vizuizi na tofauti kusudi kukaribishana na kutajirishana.

Maisha ya undani na umoja wa binadamu

Tunapoendeleza “hija ya matumaini duniani” ambayo huwakutanisha pamoja vijana kutoka nchi nyingi, tunaelewa kiundani zaidi na zaidi ukweli huu; ya kuwa binadamu wote ni familia moja na Mungu huishi ndani ya kila mtu”. (Bruda Alois, Barua kutoka Kolkata)

Kwa Bruda Roger, haikuwa lazima kuanzisha uamsho kwa jumuiya hii. Ila, baada ya kushiriki katika hatua yoyote ya hija hii ya matumaini, kila mtu anakaribishwa kurudi nyumbani na kuyaishi yale aliyoyapata kutoka kwenye injili; na kufanya hili kwa ufahamu ulioongezeka wa uzima ambao unaishi ndani yao na mazoea ya mshikamano ambao vijana hukutana pamoja mara kwa mara kusali pamoja na nyimbo kutoka Taize, hali wakibaki kuungana na ukweli kuhusu makanisa yao.

JPEG - 29.8 kb

Wakati wa mikutano hapo Taize, inaporuhusu, mabruda hutembelea vijana hawa kuwasaidia katika safari yao ya maisha. Mikutano hii ni hatua ndogo katika hija ya matumaini, wanatuwezesha kudumisha mshikamano wetu ndani ya kanisa, na kutembelea makanisa yao.

Mabruda wanapenda kuunga mkono utafutaji wa amani na mapatano popote inapowezekana. Kwa njia hii, hija ya matumaini inaonekana kupanika nje zaidi na zaidi, “na hata mwisho wa nchi” (Matendo 1:8). Hivi karibuni, mikutano ya vijana imekuwa ikiandaliwa katika Asia, Kolkata, India na Amerika ya Kusini, Kochabamba, Bolivia. Mwisho wa kila mwaka, mkutano mkubwa sana hufanyika katika moja ya miji mikubwa Ulaya.

Baadhi ya mabruda wanaishi mbali na Taize, kati ya masikini sana, wanafanya kazi pamoja na wafungwa Seoul, Korea Kusini, wanawahudumia viziwi na bubu nchini Brazil, wanaleta faraja kwa wasiojiweza Bangladesh, wanawakaribisha watoto wengi Dakar, Senegal…. Uwepo wa “nyumba za Taize” ni katika msingi wa sala na maisha ya useja.

JPEG - 32.2 kb

Matumaini duniani

Kwenye sehemu hii ya tovuti matangazo ya mikutano ijayo yanaweza kupatikana, safari za mabruda katika nchi mbalimbali, na habari kuhusu mikutano iliyofanyika, pamoja na mifano hai ya umoja wa watu, na sauti za maisha ya mabruda waliopo Afrika, Amerika Kusini na Asia.

Wakati wa safari zake kutembelea mabara mengina, Bruda Alois huandaa barua ya wazi ambayo huitoa wakati wa mkutano wa Ulaya mwishoni mwa mwaka. Barua hii ni tafakari ya mikutano inayofanyika Taize na sehemu nyingine kipindi chote cha mwaka unaofuata
(Barua kutoka Kolkata)

Barua kutoka Taize, inayotolewa mara nne kwa mwaka katika lugha kumi na saba, ni njia ya kusaidia sala na tafakari, kama sehemu ya hija ya matumaini.

Habari kutoka Taize kwa barua pepe mara mbili kwa mwaka, kwa makadirio, hizi hueleza yale yanayotokea Taize na katika nchi nyingi; matangazo ya mikutano ijayo na mambo mapya katika tovuti.

JPEG - 21.9 kb
Ilirekebishwa mara ya mwisho: 22 October 2007

Watu wengi kutoka dunia nzima wanashiriki “hija ya matumaini” katika maisha yao ya kila siku…. Nyakati nyingine tunalazimika kuelekea mitazamo mipya, mbali au karibu, kugundua tumaini la injili tena na tena. Dunia yetu, ambapo mateso mengi yana leta mahangaiko, inaitaji, wanawake na wanaume wanaomulika amani ya Mungu kwa maisha yao. Hivyo tufanye maamuzi ya ujasiri katika kwenda mbele katika njia ya upendo na matumaini.

Bruda Alois
Montreal, Canada
29 Aprili 2007