Kuanzia tarehe 14 hadi 18 Novemba 2012, kutakuwa na mkutano wa kimataifa wa vijana mjini Kigali: hatua mojawapo katika safari ya imani duniani iliyoanzishwa na Bruda Roger.
23 June 2011
Ili kusaidia kufanikisha mkutano huu, itakuwa vyema kujitoa kabla na kuheshimu kuingia kwenye mtindo wa maisha ya wenyeji wetu.
Kuongeza wigo wa sala zetu na kumuomba Mungu kututayarisha ili kutambua hazina za ubinadamu zilizopo hata katikati ya vipindi vigumu ni njia muhimu ya kuanza maandalizi.
Pasi ya kusafiria na visa:Kutegemeana na utaifa wako, ni muhimu kupata visa au makubaliano ya kuipata wakati wa kuwasili kabla ya kuanza safari. Maelezo zaidi yanaweza kupatikana hapa: http://www.migration.gov.rw/
Kuchangia Gharama:Wale waishio (...)
23 June 2011
Mchango: Kwa wale waishio Kigali wachangie kwenye gharama za mkutano, wale kutoka nje ya Kigali watajigharamia gharama za usafiri kwenda Kigali na kurudi, hakuna mchango mwingine ambao utahitajika.
Mwisho wa kujiandikisha:15 Octoba, 2012 kupitia parokia yako au mlezi wa vijana
Hifadhi tangazo:
23 June 2011
Tarehe: Kuwasili, kukaribishwa na sala ya kwanza tarehe 14 Novemba 2012, kuondoka Novemba 18 2012.
Washiriki wenye umri wa kuanzia miaka 18 hadi 30.
Malazi yatatolewa na familia wenyeji, (katika kumbi za mashule/vyuo kama itakuwa muhimu).
Vyakula vya kawaida vitatolewa: kifungua kinywa sehemu ya malazi; chakula cha mchana na cha jioni mahali pa mkutano pamoja baada ya sala za mchana na za jioni. Ratiba ya Mkutano
Jumatano 14.11.2012
Kukaribiswa kati ya saa 1 asubuhi na 6 mchana na usafiri kwenda parokia wenyeji Saa 10 jioni kuondoka (...)
22 June 2011
Kushiriki katika mkutano mjini Kigali kunamaanisha kupiga hatua mbele kiroho, na kutafuta njia rahisi za kukuza imani na nia zetu. Wakati wa kujiandaa kwenda Kigali, tunaweza:
1. Kusali pamoja kwenye jumuiya au kwenye vikundi vya sala. Kutusaidia kuifanya safari yetu iwe ya kiroho, ikiunganishwa na maisha ya parokia na vikundi vyetu.
2. Tafakari na wengine “Barua toka Chile”, na haswa kwenye dhima zifuatazo: Kuchagua furaha; Njia ya kuelekea furaha ipo kwenye zawadi ya nafsi zetu, kila siku; Kukaribisha na kushirikishana msamaha wa Mungu... (...)
22 June 2011
Mabruda wa Taizé – Mkutano wa vijana Kigali Mji wa furaha, barabara ya ThikaPO Box 6517100618 Ruaraka, Nairobi, KenyaTel: +254 724 664 198 kigali taize.fr
22 June 2011
Kuanzia tarehe 14 hadi 18 Novemba 2012, kutakuwa na mkutano wa kimataifa wa vijana mjini Kigali: hatua mojawapo ya safari ya imani duniani iliyoanzishwa na mwanzilishi wa Jumuiya ya Taizé hayati Bruda Roger.
Prayer during the pilgrimage of trust in Nairobi (2008)
Hatua za hivi karibuni katika safari hii ya imani zilikuwa barani Asia (Manila, 2010), Amerika ya Kusini (mjini Santiago Chile, (...)
25 November 2008
Japhet ni mhasibu wa shule ya msingi na ni mwenyekiti wa kamati ya Haki na Amani ya kigango kilichopo Korogocho, katika maeneo masikini ya jiji la Nairobi
Peter ni afisa jamii katika mradi wa watoto wa mitaani wa Korogocho, mradi huu unasimamiwa na kanisa kuwasidia watoto wa mitaani ili kuwarudisha katika hali bora ya kijamii na kiuchumiWapendwa vijana kutoka nchi mbalimbali Duniani,
Kuanzia tarehe 26-30 Novemba mwaka huu, tunawakaribisha hapa Kenya katika tukio maalum la maombi, kushirikishana, kutafakari na tunawaalika katika makanisa (...)
10 November 2008
Wakati wa mkutano Geneva, Bruda Alois alitangaza, “Tutaendeleza mikutano ya vijana katika mabara mengine. Baada ya Asia na Amerika ya kusini (Latin America), Mwaka ujao Tutaenda Afrika. Kuanzia tar 26-30 Novemba tutakaribishwa ukanda wa chini ya Ikweta, Afrika Mashariki, nchini Kenya, katika mji wa Nairobi.Utoaji msaada kwa wakristo Kenya
Kwa kipindi cha muda wa siku chache zilizopita, baadhi (...)