Safari kwenda Taizé
Taizé ipo nje ya barabara ya A6, katikati ya Chalon-sur-Saóne na Mácon. Kituo cha karibu cha treni, Mácon Loché, kipo umbali wa saa 1 na dakika 35 kwa TGV (treni ya mwendo kasi) kutoka Paris. Ni mwendo wa masaa 2 kwa gari kutoka Geneva. Ramani yetu inaonesha mahali penyewe na maelezo zaidi juu ya njia nyingine za kuelekea Taizé katika eneo hilo.
Kuna ratiba za treni pamoja na mabasi ya kuunganisha; maelezo kuhusu huduma za kawaida za mabasi ya kwenda Taizé kila mwishoni mwa wiki, kutoka nchi mbalimbali; jinsi ya kufika Taizé kutoka viwanja vya ndege vya karibu – CDG Paris, Lyon na Geneva; teksi na mabasi ya kukodi hapa Taizé na maeneo ya jirani; na, kwa mara ya kwanza nchini Ufaransa, katika kiwanja cha ndege cha CDG Paris kuna melezo ya hatua kwa hatua jinsi ya kufika Taizé kutoka kiwanjani kwa wasiozungumza kifaransa.