TAIZÉ

Kwa nini Bruda Roger aliuawa

 

Katika jumbe tulizopokea mwaka uliopita, watu walilinganisha kifo cha bruda Roger kama kile cha Martin Luther King, askofu mkuu Romero au Gandhi. Haiwezi kukataliwa kwamba palikuwa na tofauti pia. Watu hao walijihusisha katika mapambano ya kisiasa na kifikra, waliuliwa na wapinzani ambao hawakuweza kuvumilia hoja zao au ushawishi wao.

Wengine wanaweza kusema ni bure kutafuta kuelewa mauaji ya bruda Roger. Uovu sikuzote unapinga maelezo. Mtu mwenye haki katika agano la kale alisema kwamba alichukiwa “bila sababu” na mtakatifu Yohane aliweka maneno hayo hayo mdomoni mwa Yesu: “walinichukia bila sababu”.

Katika kuishi karibu na bruda Roger, kitu kimoja kuhusu tabia yake huwa kinanigusa, pia inanishangaza kama hii sio sababu ya kuwa kwa nini alikusudiwa kuuawa. Bruda Roger alikuwa hana hatia. Sio kwamba hakuwa na mapungufu. Ila asiye na hatia ni yule ambaye anashuhudia vitu kwa namna ambayo havionekani kwa wengine. Kwa wasio na hatia ukweli ni kitu dhahiri. Hautegemei sababu yeyote. Wanauona, kwa namna Fulani, ni vigumu kwao kugundua kuwa, watu wengine wanatumia njia za maumivu zaidi kuufahamu. Wanapokitamka ni kirahisi na kinaeleweka kwao, lakini wanashangazwa kuwa wengine hawaguswi kwa namna ile ile. Nirahisi kuelewa kwanini watu hawa huhisi kupotea au kuwa katika hatari. Na pia kawaida kutokuwa kwao na hatia sio kwamba hawana ufahamu wa mambo. Kwao, ukweli sio kiza kama ilivyo kwa wengine. Wao huuona.

Nichukue mfano wa umoja wa Kikritu. Kwa bruda Roger, ilikuwa ni dhahiri kwamba, kama Kristu alitaka umoja huu, basi ilitakiwa watu waanze kuuishi bila kuchelewa. Malumbano yaliyokuwa kinyume na wito huu wa Kristu wa umoja hakuyaona kuwa ni sawa. Kwa Bruda Roger, umoja wa Kikristu juu ya yote ni suala la upatanisho. Na mwishoni alikuwa na haki, kwa wale tuliobaki tunajiuliza maswali kila mara kama tunaweza kulipa gharama za umoja. Je umoja ambao hautugusi miili yetu unastahili jina?

Ilisemwa kipindi fulani kwamba hakuwa na teolojia. Lakini je, yeye hakuwa na mtazamo halisi zaidi ya waliosema hilo? Kwa karne nyingi, Wakristu walijaribu kujaribu kujengea hoja utengano wao. Walikuza hoja za upinzani wao pasipo sawa. Bila kugundua kwamba waliingia katika uadui na hawakuona hili likitokea machoni pao. Hawakuona kabisa. Umoja ulionekana hauwezekani kwao.

Bruda Roger alikuwa mhalisia. Alitilia maanani kile kilichoshindikana, hasa fikra za umoja. lakini hakuishia hapo. Usafi wake ulimpa msukumo ambao ulikuwa wa kipekee, aina ya ukarimu ambao haukukubali kushindwa. Hadi mwisho, aliona umoja wa Kikristu kama suala la upatanisho. Sasa upatanisho ni hatua ambayo kila Mkristu anaweza kuichukua. Kama kila mmoja angeichukua, umoja ungepatikana.

Kuna sehemu nyingine ambapo utendaji wa Bruda Roger ulionekana na labda ilionekana zaidi katika msingi wa tabia yake: hakuweza kuvumilia kitu chochote kilichovuta upendo wa Mungu. Hapa, tunagusa ufahamu wa kweli za Mungu. Si kwamba alikataa kutafakari, ila alijisikia kwa nguvu ndani yake kwamba namna fulani ya kuongea ambayo ilipenda iwe sahihi – kwa mfano kuhusu Upendo wa Mungu – katika hali halisi haikueleweka kwa watu wasiofahamu wanaotegemea kutoka upendo huo.

Kama Bruda Roger alisisitiza sana kwenye uzuri usiosemeka wa binadamu, hii inatakiwa ionekane katika mwanga ule ule. Hakuwa na hisia mbovu kuhusu uovu. Kwa asili alikuwa katika hatari. Lakini alikuwa na uhakika kwamba kama Mungu anapenda na kusamehe maovu yetu, basi kwake yeye yameisha. Msamaha wa kweli unaviamsha vilindi vya moyo wa binadamu, ambavyo vimeumbwa kwa ajili ya wema.

Paul Ricœur aliguswa na msisitizo katika wema. Siku moja alituambia hapa Taizé kwamba aliona hapo aliona maana ya dini. “kuweka huru vilindi vya wema ndani ya watu, na kwenda kutafuta sehemu ambazo umezikwa kabisa”. Zamani, namna fulani ya mahubiri ya Kikristu yaliurudia uovu wa asili wa ubinadamu. Ilifanya hivyo ili kuhakikisha kwamba msamaha uonekane kuwa ni wa bure na bila mastahili. Lakini hii iliwaondoa watu wengi katika imani; hata kama walisikia upendo ukiongelewa, walikuwa na hisia kwamba sehemu fulani ya upendo ilifichwa na kwamba msamaha uliotangazwa haukuwa kamili.

Kitu cha thamani kuliko vyote Bruda Roger alituachia labda kinaweza kupatikana hapo: ni kwamba hisia ya upendo na msamaha, kweli mbili ambazo ni dhahiri kwake na alizishika kwa umoja ambao hatukuuelewa. Katika eneo hilo alikuwa mkweli kabisa – mara zote wa kawaida, asiyefuata ushawishi, alisoma nyoyo za watu, na alikuwa na uwezo wa kuwa na matumaini mazito. Uzuri wa macho yake uliweza kuelezea hayo. Kama alijisikia nyumbani akiwa na watoto ni kwa sababu waliishi kwa njia hiyo hiyo ya moja kwa moja, hawawezi kujilinda na hawawezi kuamini kitu ambacho ni kigumu, na mioyo yao inayafuata moja kwa moja yale yanayowagusa.

Wasiwasi haukukosekana katika maisha ya bruda Roger. Kwa sababu hiyo alipenda maneno haya: “usiruhusu giza langu liongee nami!”. Giza lilimaanisha kushawishiwa na wasiwasi. Lakini wasiwasi huu hausumbui ule ushahidi wa Upendo wa Mungu alijiosikia ndani. Labda ni wasiwasi ambao ulihitaji lugha inayoeleweka. Ushahidi wa ndani ninaouongelea haukupatikana kwa ngazi ya elimu, ila ulipatikana kwa undani zaidi kwenye ngazi ya moyo. Na kama vile isivyowezekana kila kitu kulindwa kwa nguvu za hoja au namna nzuri ya kutengenezwa, uwazi huu haukuwa imara.

Katika injili, urahisi wa Yesu unastaajabisha. Baadhi ya waliomsikiliza walijisikia wakizungumziwa. Ilikuwa kama vile mawazo ya ndani kabisa ya mioyo yao yamewekwa wazi. Lugha rahisi ya Yesu na uwezo wake wa kusoma mioyo ilileta hali ya utisho ndani yao. Mtu ambaye haruhusu wao wafungiwe katika malumbano alionekana hatari kwa baadhi. Mtu wa aina hiyo anastaajabisha, lakini hali hii inaweza kirahisi kugeuka kuwa uadui.

Bruda Roger aliwavutia watu kwa wema wake, uelewa wake wa haraka, mwonekano wake. Nafikiri aliona ndani ya macho ya baadhi ya watu, kwamba mshangao unaweza kugeuka kuwa hali ya wasiwasi au hasira. Kwa mmoja anayebeba malumbano ndani yake, basi hali yake ya kuwa mkweli isingeweza kuvumiliwa. Na kwa namna hiyo haikuwa inatosha kuivunja hali hii. Hali hii ilatakiwa iondolewe. Daktari Benard de Senarclens aliandika, “kama mwanga ni mkali sana, nafikiri ule uliotoka kwa bruda Roger ingeshindikana kuuangalia, ambao mara nyingi sio rahisi kuupokea. Basi ufumbuzi pekee ni kuzima chanzo kinachotoa mwanga huu”.

Nilitaka kuandika tafakari hizi kwa sababu zinawezesha kuleta hali ya umoja wa maisha ya bruda Roger. Kifo chake kilileta fumbo kutokana kwa jinsi alivyokuwa. Hakuuawa kwa ajili ya kitu alichokitetea. Aliuawa kwa ya alivyokuwa.

Bruda François wa Taizé

Ilirekebishwa mara ya mwisho: 26 September 2007