TAIZÉ

Bruda Alois 2010

Barua Kutoka China

 

Katika kila binadamu kuna hangaiko

Ingawa tofauti ya tamaduni yaweza kutengeneza mipaka kati ya mabara, binadamu wote ni famila moja [1]. Safari yetu ya China imeipa nguvu udhihirisho huu ndani yetu. Licha ya tofauti ya tamaduni zetu, umri wetu au historia yetu wote tuna hamu, tuna kiu ya uhai tele.

Mara nyingi Biblia huzungumzia kiu hiyo. Biblia uona kiu hiyo kama alama iliyowekwa ndai yetu na Mungu ili kutuvutia kwake [2]. Je, tunawezaje kukubali kiu hii ituchimbe, bila kutafuta njia za haraka za kuiridhisha [3]? Hii yaweza kuwa upendo unaowaka ndani yetu kwa yule ambaye ni zaidi ya uwezo wetu wote kumfahamu yaye [4].

Tunavyozidi kumtafuta Mungu, ndivyo tunavyoweza kustajabishwa na utambuzi huu: Mungu ndiye anayeanza kututafuta. Katika kitabu cha nabii Hosea, Mungu anawazungumzia watu wake kama Mwanaume kwa mpenziwe: “Nitamshawishi, nitampeleka Jangwani na kusema na moyo wake.” Alafu anaongeza, “ Nitakufanya mke wangu milele... kwa fadhili na huruma. [5]

Tamanio hili la Mungu linakuwa mwili na damu halisi katika Yesu [6]. Kristu alilipa kwa kutaka kukaa nasi milele: kwa kifo chake msalabani, alijinyenyekeza hata kuhukumiwa bila hatia. Sasa amefufuka toka wafu anamtuma Roho mtakatifu aliyepo bila kuonekana ambaye anatusukuma kwenye ukamilifu wa Mungu.

Kutenganisha tamaa zetu

Moyo wa binadamu ufurika kwa wingi wa tamaa na maazimio; tunataka vitu vingi, wakati mwingine vitu vinavyopingana. Lakini tunajua kuwa hatuwezi kufanya au kuwa na kila kitu. Mbali ya kutukatisha tamma kwa huzuni, utambuzi huu unaweza kutuweka huru na kutusaidia kuishi bila vipangamizi. [7]

Ndiyo, ni muhimu kutenganisha tamaa zetu. Siyo zote ni mbaya na siyo zote ni nzuri pia. Tunatakiwa kuwa wavumilivu kufahamu ni zipi tuzitimize na zipi tuziweke kando.

Kuamua ni maazimio yapi tuyape kipaumbele, kuchunguza yale yaliyomo ndani mwetu, tayari ni njia ya kumsikiliza Mungu. Mungu anazungumza nasi kupitia matamanio yetu. Ni juu yetu kusikiliza sauti yake kati ya sauti nyingi zilizomo ndani mwetu. [8]

Kuamsha ndani mwetu tamaa ya Mungu

Ni lazima kuacha hamu ya kina kabisa iamke ndani mwetu: tamaa ya Mungu!

Ni kweli kuendeleza roho ya mshangao na yakuabudu ni vigumu, kwakuwa jamii yetu inatia mkazo kwa kufanya mambo kwa ufanisi na kwa muda mfupi iwezekanavyo. Lakini kwenye kipindi cha ukimya, wakati kunaonekana hakuna kinachofanyika ndani mwetu, Roho mtakatifu anafanya kazi bila sisi kufahamu.

Kujua jinsi ya kusubiri... Kwa kuwepo tu bila ya kuwa na sababu nyingine. Kupiga magoti, kutambua uwepo wa Mungu. Kufungua mikono yetu kwa tendo la kukaribisha. Kujinyamazisha tayari ni kielelezo cha uwazi kwa Mungu.

Matendo ya kusifu na tafakari vimekuwa sehemu ya tamaduni za Asia kwa karne. Je, wakristu wanawezaje kuathiriwa na uvutio wa kidunia kutafuta ujasiri wa kufufua sala za kale? Katika liturujia na mikusanyiko, hali ya undani yaweza kuunganishwa na hali ya ujumuia na sherehe.

Kushirikishana tuliyonayo

Kuacha kiu ya Mungu ituingie haitutengi na mahitaji ya dunia inayotuzunguka. La hasha! hii kiu inatuongoza kufanya yote tunayoweza ili wengine wafurahie motokeo bora ya uumbaji na kufurahia kuishi. [9]

Kutenganisha tamaa zetu kukubali kutokuwa na kila kitu, kunatupelekea kuto jilimbikizia mali. [10] Katika karne ya nne, tayari Mtakatifu Ambrosi alikwisha sema, “Siyo mali yako ambayo unagawia masikini; unachofanya ni kuwarudishia”.

Kujifunza kutokuwa na kila kitu kunatuzuia kujitenga, ustawi wa mali mara nyingi hufuatana na kujiangalia ndani bila mawasiliano ya kweli. Haitachukua mengi mambo kugeuka [11].

Fursa nyingi za kushirikishana ziko ndani uwezo wetu: kutengeneza mitandao ya kusaidia na kuendeleza uchumi kwa mshikamano, kukaribisha wahamiaji, kusafiri ili kuelewa tamaduni nyingine na mazingira mengine ya binadamu kutokea ndani, kunawezesha mahusiano kati ya miji, vijiji au parokia, ili kusaidia wale wahitaji, kutumia teknolojia mpya vizuri kutengeneza usaidiaji wenye manufaa kwa wote.

Lazima tuwe makini haswa kutozidiwa na matazamio hafifu ya baadae kwa kuangalia habari mbaya. Vita siyo lazima [12]. Heshima kwa wengine ni thamani mno katika kuandaa amani. Mipaka ya nchi tajiri lazima iwe wazi zaidi. Haki kuu duniani inawezekana [13].

Tafiti nyingi na miito ya kuendeleza haki na amani ipo, kinachokosekana ni msukumo muhimu kustahimili zaidi ya nia njema.

Injili inatuita kukumbatia maisha ya urahisi kunatufungua mioyo yetu kushirikishana na furaha, itokayo kwa Mungu.

Kuongeza imani kwa Mungu

Wakati imani inaonekana inatoweka katika jamii nyingi, hamu ya kiroho inazaliwa. Tunahitaji kutafuta maneno sahihi, yaliyo mepesi, kuifanya imani inayotupa uhai iwafikie wengine.

Watu wengi hawawezi amini Mungu anawapenda jinsi walivyo. Kwa wengine, majaribu mengi yamewafanya washindwe kuwa na imani na Mungu [14]. Tunawezaje kueleza kwa uwazi kuwa Mungu yuko makini juu ya wasiwasi na uhasi kwa yale yasiyo na maana [15]? Yesu mwenyewe alishiriki mateso ya wale wote waliokuwa wanateseka, alilia msalabani, “Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha? [16]

Watoto wengi wanakua bila kuwa na mtu wa kuwaambia kuwa Mungu anawapenda. Kijana gani ataambatana naye au nao kenye njia ya imani?

Kwenye kuingia utu uzima, kuna wale ambao wanapoteza uhusiano na jumuia ya wakristu. Mara nyingi siyo kwa uchaguzi makusudi ila mfululizo matukio unasukuma imani chini ya mlolongo wa vipaumpele. Je, marafiki wanawezaje kusaidiana kufufua uhusiano na jumia ya waumini?

Wakati mwingine pengo huongezeka kati ya ufahamu katika uwanja wa imani na ile iliyopatikana katika uwanja mwingine. Imani ambayo inabikia katika usawa wa misemo iliyoufundishwa wakati wa utoto inakuwa ngumu kukabiliana na maswali ya ujana. Tunaweza kupata furaha katika kuongeza uelewa wetu wa fumbo la imani katika kila hatua ya maisha yetu. [17]

Kufufua ushupavu wetu

Mungu anatuita kuuabadili ulimwengu kwa jitihada yenye nguvu lakini kubwa vile vile kwa unyenyekevu mkubwa.

Wakubwa wanaweza kuwapa moyo vijana, kizazi kipya kina uwezo sawa na waliowatangulia.

Mabadiliko haya lazima yaanze na sisi wenyewe: lazima tumuache Yesu mfufuka abadilishe mioyo yetu, na kumruhusu Roho mtakatifu kutuongoza kwenye kina kirefu ili tuweze kwenda mbele kwa ushupavu.

Tufurahi katika kiu ambayo Mungu ameweka ndani yetu! Inatupa moyo mpya katika nguvu tendaji katika maisha yetu yote. “Mwache yeyote mwenye kiu aje: Mwache yeyote anayetamani kupokea maji ya uhai, bure”. [18]

Unaufanyia nini uhuru wako?

Ulaya na sehemu nyingine za dunia, swali hili linaulizwa kwa msisitizo zaidi.

Miaka ishirili iliyopita, kabla tu ya mabadiliko makubwa Ulaya, tuliweza kuvuka vikwazo vingi na kuandaa mikutano miwili ya vijana huko Ulaya ya kati.

Mkutano wa vijana wa Mashariki-Magharibi mjini Pécs, Hungary. Wakati vijana wanakusanyika, “Pazia la chuma” kati ya Hungary na Austria lilifunguliwa na kote barani Ulaya.

Mkutano wa Ulaya mjini Wroclaw, Poland. Wakati wa maandalizi ya mkutano huu, ukuta wa Berlin ulidondoka, kuwezesha zaidi ya vijana 50,000 kutoka kote barani Ulaya kukusanyika kwa uhuru kwa mara ya kwanza.

Huko Wroclaw bruda Roger aliwaambia washiriki,“ kipindi hiki watu wengi wameona pazia la chuma likidondoka na wakati huo huo kuta uwoga na fedhea zikidondoka. Kwahiyo katika wiki za hivi karibuni, watu wengi wamekuwa wakisali mchana na usiku kwa uhuru wa watu”.

Miaka ishirini Baadae, mwaka 2009, mikutano mitatu imewaleta pamoja vijana: mwezi Mei mjini Vilnius (Lithuania), Oktoba mjini Pécs (Hungary) na mwisho wa Disemba mjini Poznan (Poland) kwa mkutano wa Ulaya.

Katika tukio hili, tungependa tujiulize swali: leo, ulaya pia kwenye mabara yote, je, tunatafakari vya kutosha maana ya uhuru? Kila kijana anaweza kujiuliza: ninautumiaje uhuru wangu?

Acha ushibishwe kwa neno la Mungu na kusali pamoja

Nchini China, tulikutana na makundi ya wakristu ambao wanatambua sana hazina, ambayo ni Biblia [19]. Baadhi wangependa kuisoma zaidi, ila kwa kawaida siyo rahisi. Pamoja nao, sisi tunaitwa kutambua njia hizi mbili:

- Kiini cha Biblia ni upendo wa Mungu. Kati ya Mungu na ubinadamu kila kitu kinaanza na ubichi wa pendo wa kwanza; kisha vinakuja vikwazo na hata kukosa uaminifu. Lakini Mungu hachoki kutupenda, mara zote anaedelea kututafuta watu wake. Biblia ni hadithi ya uaminifu wa Mungu.

- Mungu anajitoa kwetu kupitia Yesu, yeye ni Neno la Mungu. Tunaposoma Biblia tunakutana nae, Kristu; tunasikia sauti yake; tunaingia katika uhusiano nae [20].

Katika kusoma, tunaweza kushika neno moja tu. Jambo la muhimu ni kulifanyia kazi. Katika njia hiyo tunaweza kulielewa vizuri zaidi na zaidi.

Nchini China, pia tulisali na wakristu, tuliimba nyimbo za Taizé katika lugha yao. Wengine walituuliza ni jinsi ya kufanya sala na wengine. Tulishilikishana nao baadhi ya mambo kwa undani, yalisukumwa na uzoefu katika jumuia yetu. Kwa kweli yanatakiwa kuwa patanifu na mazingira ya kila kanisa husika.

- Kufanya mahali pa sala pawe panavutia kwa kutumia mbinu rahisi, ili pawezeshe kuabudu.

- Kuhakikisha sala inaendelea vizuri: nyimbo, zaburi, somo, wimbo, ukimya (dakika 8 mpaka 10), maombi, Baba yetu, sala ya mwisho, nyimbo.

- Wakati wa sala, soma fungu fupi la Biblia ambalo ni rahisi kuelewa, kuweka kando masomo magumu kwa ajili ya maelezo nje ya sala za pamoja.

- Imba sentensi moja ya maandiko au mapokeo, kurudia mara kwa mara, ili ijenge mizizi ndani yetu. Kifungu cha maandiko kinachoimbwa huwa rahisi kujifunza kwa moyo na kinaweza kuwa nasi mchana na wakati mwingine usiku.

- Tumia ishara rahisi: Ijumaa jioni kwa mfano, weka kiashirio cha msalaba chini. Kila mmoja anaweza kuweka paji lake la uso kwenye msalaba, kitendo hiki kinaashiria kuwa wanamwachia Kristu mizigo yao na maumivu ya dunia. Siku ya Jumamosi jioni, soma Injili ya Ufufuko wakati watoto wanawasha mishumaa midogo ambayo kila mmoja amepewa, kuashiria kwa wote mwanga wa Pasaka.

Ilirekebishwa mara ya mwisho: 17 June 2010

Footnotes

[1Sisi sote ni familia moja, tunoishi katika sayari moja, hivyo ni muhimu kuwajibika kwa haraka kwa ajili ya mazingira na uumbaji wote.

[2Ee bwana, Mungu wangu, nitakutafuta mapema, nafsi yangu inakuonea kiu, mwili wangu wakuonea shauku, katika nchi kame na uchovu, isiyo na maji (Zaburi 63:1), kwa nafsi yangu nimekutamani wakati wa usiku, naam, kwa nafsi yangu ndani yangu nitakutafuta mapema. Maana hukumu zako zikiwapo duniani. Watu wakaao duniani hujifunza haki (Isaya 26:9).

[3Tunaweza kutamanishwa kutimiza mataminio yetu kijuujuu. Je, si ulafi ni njia ya kutojishughulisha na maswali ambayo tunaogopa kuyafikiria mpaka mwisho?

[4Katika karne ya nne, mtakatifu Gregori Nazianzen aliimba maajabu ya Mungu; “Ee wewe, ambaye ni zaidi ya vyote, twawezaje kukuita kwa jina lingine? Wimbo gani tunaweza kukuimbia? Hakuna maneno yanayoweza kukuelezea wewe.... Shauku ya wote; maumivu ya wote, unatusukuma kwako. Wakati huo huo mtakatifu Agustino aliandika, “Kupitia hamu yetu, Mungu anongeza tamaa; kwa tamaa, anachimba roho. Kwa kuchimba anaiwezesha roho kutamani.”

[5Tena siku hiyo itakuwa asema Bwana utaniita Ishi; wala hutaniita tena Baali; tena itakuwa siku hiyo Mimi nitaitika, asema Bwana, nitaziitikia mbingu, nazo zitaiitikia nchi. (Hosea 2:16, 21)

[6Siku moja Yesu alimuuliza mwanamke kando kando ya kisima, “Naomba maji ninywe” (Yohana 4:7), Hadithi inavyoendelea inaonyesha kuwa, alikuwa na kiu ya kueleza zawadi ya Mungu. Kwenye msalaba atasema tena, “Nina kiu” (Yohana 19:28). Kulingana na mazingira, Je, kiu hii siyo kielelezo cha mwisho ya tamaa ya Yesu kutoa uhai wake namna hii?

[7Je, siyo muhimu kujifunza kukabiliana na upungufu na hali ya kutotabilika kwa maisha yetu? Jamii, zenye mafanikio mara nyingi hujaribu kuficha ukweli huu. Madhumuni makuu yanakuwa kuficha udhaifu, kusahau mapungufu ya ndani, maumivu na kifo ni sehemu ya maisha.

[8Nitamhimidi bwana aliyenipa shauri, naam mtima wangu umenifundisha usiku (Zaburi 16:7)

[9Imani haihusiani na anga za kidini tu. Hakuna chochote ambacho kinaweza kuathiri ubora wa maisha ambacho kinatuacha tukiwa hatujali. Utafiti wa sayansi, kielelezo cha sanaa, siasa, muungano wa kibiashara, majukumu ya kijamii vyaweza kuwa na nia ya kumtumikia Mungu. Kujifunza, kufundisha, kuendesha biashara kwa utu, kutoa nafsi zetu kwa familia, kupanua urafiki, vyote hivi vyaweza kuandaa ujio wa ufalme wa Mungu.

[10Mabadiliko ya uchumi wa ulimwengu na mfumo wa fedha hauwezi kuja bila mabadiliko ya moyo wa binadamu: Je, misingi ya mifumo yenye haki inaweza kujengwa wakati baadhi wanaendelea kutaka kujilimbikizia mali kataka hasara ya wengine?

[11Wakati shirika letu linaandaa mikutano ya vijana kataka miji mikubwa kwenye mabara tofauti, kama hatua za “Safari ya imani duniani”, tunakaribisha maelfu ya familia kukaribisha kijana mmoja au zaidi, hawajui ni lugha gani wataongea. Tunaona inahitaji kidogo tuu kuweka wazi uzuri uliopo ndani ya moyo wa binadamu.

[12Pamoja na uwoga na wakati mwingine makosa, mwanzo wa karne ya ishirini na moja umekuwa na ukuaji wa utambuzi wa kimataifa na utafutaji wa upangaji makini wa mahusiano kati ya watu: ukusanyaji wa maoni ya halaiki, majaribio ya kukabiliana na changamoto kwa pamoja (hali ya hewa, mazingira, afya, uchumi)... Ongezeko la utegemeano kati ya mataifa yaweza kuongeza uwoga, kuamsha majibu ya kujikinga kuonyesha utambulisho. Lakini haiwezi kuwa dhamana ya amani?

[13Bado kuna watoto milioni tisa duniani, walio chini ya umri wa miaka mitano ambao hufa kila mwaka, na asilimia 29 ya watoto amabo huishi katka nchi zanazoendelea ni waathiriwa wa utapia mlo. Hii haikubaliki kabisa. Wakati huo huo, kusitizia hilo, shukrani kwa makubaliano ya haki za mtoto, yaliyopitishwa kwa kishindo na balaza la umoja wa mataifa mwaka 1989, kumekuwa na mabadiliko jinsi watoto wanavyotendewa, kwa juhudi za kimataifa, vifo na utapia mlo umepungua kwa karibu ya asilimia thelasini katika miaka ishirini iliyopita.

[14Hii siyo tu kwa wale wanaopitia majaribu mengi. Nafikiria kuhusu kijana mmoja ambaye wakati mwingine nakutana nae Taizé. Ana ugonjwa usiowezekana kutibika ambao unazidi kuongezeka. Anaumwa sana. Tayari fursa nyingi za kutimiza maisha zinatoweka. Lakini cha kushangaza, kwa kuangalia kwenye macho yake na mtazamo wake mzima yupo wazi. Siku moja aliniambia, “Sasa nafahamu maana ya kuamini. Zamani sikuhitaji, lakini sasa nafahamu”. Na aliongeza kwenye barua aliyoniandikia, “Sitakiwi kuacha ugonjwa wangu kuchukua muda, nafasi, usikivu na wakati wangu wote”. Kisha nikajiambia: laiti huyu kijana angejua jinsi gani maneno yake yanavyoniwezesha kuendelea na jinsi gani yanavyowezesha wengine kwa mtazamo wake. Ndani yake kuna taswira ya unyenyekevu lakini halisi ya fumbo la ufufuko.

[15Kati ya vitabu vinavyounda Biblia na hata vitabu vingine vitakatifu vya dini nyingine, hakuna kinachoelezea kupinga kwa nguvu maumivu ya mtu asiye na hatia kama kitabu cha Ayubu. Ayubu anakataa upumbavu wa maisha ya mateso, na analalamika kuhusu dunia kuwa ingekuwa vyema kama asingezaliwa. Lakini hata katikati ya haya mapingano anazungumza na Mungu. Ajibiwi maswali yake yote, lakini anapata amani katika kukutana na Mungu.

[16Na saa tisa Yesu akapaza sauti yake kwa nguvu, “Eloi, Eloi lama sabakthani?”; maana yake “Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha?” (Marko 15:34)

[17Njia zipo: Vikundi vya Biblia, masomo mafupi ya Biblia kila siku, muda wa ukimya na mafungo, mafundisho katika parokia, mafundisho kwa kushirikiana na idara ya theolojia au vitengo vingine katika kanisa, Mafundisho kwenye intanet.

[18Na roho na bibi harusi wasema, “Njoo” naye asikiaye na aseme, “Njoo”, naye mwenye mwenye kiu na aje; na yeye atakaye na ayatwae maji ya uzima bure. (Ufunuo 22:17)

[19Kote duniana, kuna mifano mingi ambayo inaonyesha jinsi gani Biblia imekuwa inapendwa, jinsi ilivyoingia ndani ya binadamu na umbali gani huu upendo unaweza kumpeleka mtu. Nchini Latvia, mwaka 1940, padri aitwaya Victor alikamatwa kwasababu alikuwa na Biblia. Mwakilishi wa utawala aliitupa Biblia chini na kumwamuru padri aikanyage. Akapiga magoti na kuibusu. Kisha akakamatwa na kuhukumiwa miaka kumi ya kazi ngumu Siberia.

[20Kuzungumzia maandiko, askofu mmoja nchini Ufillipino alisema, “Mungu anongea, lakini pia anasikiliza, haswa kwa wajane, yatima, wateseka, maskini, ambao hawana sauti. Kwahiyo kuelewa neno la Mungu, ni lazima tujifunze jinsi anavyosikiliza”.