TAIZÉ

Ya 2006

Barua ambayo haijakamilika

 
Adhuhuri ya ile siku aliyofariki, Agosti 16, Bruda Roger alimwita mmoja wa mabruda na kumwambia, “Nakili maneno haya kwa makini.” Kulikuwa na kimya kwa muda alipojaribu kufikiri jinsi atakavyopanga maneno yake. Kisha akaanza “Katika ile hali ambayo jamii yetu imezindua uwezekano katika familia ya mwanadamu kuongezeka…….”Kisha akaachia hapo akiwa amechoka kiasi ambacho hangeweza kuimalizia ile sentensi.

Maneno haya yanaashiria ujasiri aliokuwa nao hata katika ukongwe wake. Ni nini alichomaanisha kwa kusema “kuongezeka”? Bila shaka alitaka kusema: Jaribu iwezekanavyo ili upendo wa Mungu utambulike kwamba niwa kila mmoja na bila kubagua ni kwa wote. Alitaka jamii yetu ilete fumbo hili kwa mwanga kupitia kwa maisha yake katika ile hali ya kujitolea kwa unyenyekevu na kwa wengine. Kwahivyo, sisi mabruda tunalichukua changamoto hili pamoja na wale wote wanaoitafuta amani duniani kote.

Wiki chache kabla ya kifo chake, alikuwa ameshaanza kutafakari kuhusu barua ambayo ingesomwa kwa mkutano wa adhara wa Milano. Alikuwa amenakili maudhui na masomo kadhaa ambazo angetaka kuyashughulikia katika kazi yake. Tumeyachukua jinsi yalivyokuwa ilituunganishe “Barua ambayo haijakamilika”, ambayo imetafsiriwa kwa lugha hamsini na saba (57). Hii ni kama habari ya mwisho kutoka kwa Bruda Roger, ambayo itatusaidia katika safari ambayo Mungu “anaiongoza hatua kwa hatua.
(Zaburi 18:36)

Tunapotafakari kuhusu barua hii ambayo haijakamilika katika mikutano iliyoandaliwa mwaka huu wa 2006 kule Taizé, wiki kwa wiki au mahali popote katika mabara tofauti tofauti, kila mmoja anaweza kujaribu kutafuta njia ya kuikamilisha katika maisha anayoishi.

Bruda Alois

“Nawaachieni amani; nawapeeni amani yangu.” [1] Ni amani ipi hii ambayo Mungu anatupa?

Kwanza kabisa ni amani ya ndani, amani iliyo Moyoni. Amani hii inatuezesha kuitazama ulimwengu kwa matumaini, hata ingawa imegawanywa kwa vita na migogoro.

Hii amani kutoka kwa Mungu, pia inatusaidia ili tuweze kuchangia kwa unyenyekevu, kuileta amani mahali ambapo imesambaratika.

Amani ya dunia ni ya dharura kwa kupunguza mateso, na hasa ili wana wa leo na wa kesho wasiishi kwa dhiki pamoja na ukosefu wa usalama.

Katika injili yake iliyo na utabiri, Yohana Mtakatifu anahimiza kumtambua Mungu kwa maneno matatu “Mungu ni pendo”. [2] Ikiwa tutayazingatia maneno haya matatu, tutaweza kunawiri hata zaidi.
Ni msisimko upi tunaoupata kutokana na maneno haya?

Hata ingawa hisia na amani zinadhihirika, Mungu hakumtuma mwanae wa pekee Yesu Kristu duniani kumdhihaki yeyote ule, bali kila mwanadamu aweze kufahamu kuwa yeye anapendwa sana na kwamba aweze kutambua umoja wake na Mungu.

Lakini mbona watu wengine wanashangazwa na maajabu ya upendo na kwamba wanapendwa? Na kwa nini wengine wana hisia ya kuwa wametengwa?

Kila mtu angetambua ya kwamba Mungu yuko ndani yake hata katika upweke wake.Mungu asema kwa kila mwanadamu “unadhamana mbele yangu, nakupenda sana.” [3] Kweli, yote ambayo Mungu anaweza kukutendea ni kukupa upendo; ambao umejumuishwa katika injili yote.

Kile ambacho Mungu anatuuliza na ametujalia ni huruma yake.Wakati mwingine ni vigumu kutambua ya kwamba Mungu anatupenda. Lakini tukigundua kuwa upendo wake ni msamaha zaidi ya yote, mioyo yetu hupata amani na hata kubadilika.

Vilevile, kwa Mungu tunapata kusahau yale yote yanayo sumbua mioyo yetu: hii ndio chemichemi ambayo kwake tutaweza kuwa na nguvu hata zaidi.

Tunafahamu kuwa Mungu anatuamini sana kiasi cha kwamba ana wito kwa kila mmoja wetu? Wito huu ni upi? Mungu anatualika tuwe na upendo jinsi anavyotupenda. Hakuna upendo mwingine mbali na ule wa kujitolea zaidi kwa Mungu na kwa wengine.

Yeyote ambaye maisha yake yana msingi wa Mungu, huchagua kuwa na upendo. [4]

Na moyo ulioamua kuwa na upendo waweza kuongeza uzuri usio na kipimo. Yeyote anayeonyesha upendo kwa uaminifu, maisha yake huwa na amani ya kupendeza.

Wote wanaoamua kupenda na kuyasema kwa maisha yao, hujiuliza swali hili: tutawezaje kupunguza uchungu na mateso ya wengine hata ikiwa wako karibu au mbali nasi?

Lakini ni nini maana ya upendo? Yaweza kuwa ni kushiriki mateso ya wale wanodhulumiwa zaidi? Ndio, ni hivyo.

Tena, ni nini maana ya upendo? Maana ya upendo ni kusameheana na kuishi kama watu waliopatanishwa. [5]
Mara kwa mara upatanisho huleta uchangamfu moyoni.

Katika kijiji kimoja kilichokuwa mlimani mahali nilipozaliwa, kuliishi familia kubwa iliyokuwa maskini. Mama yangu alikuwa ameshaiaga dunia. Kijana mmoja aliyekuwa mdogo kuniliko alikuwa akitutembelea mara kwa mara. Alimpenda mama yangu kana kwamba alikuwa wake. Siku moja aligundua kuwa walikuwa na mpango wa kukihama kijiji kile na kwake, haikuwa rahisi kamwe kuhama.

Wawezaje kumfariji mtoto wa miaka mitano au misita? Ilikuwa kana kwamba hakuwa na mbinu aliyohitaji ili kuonyesha madhumuni ya utengano huo.

Kristu bado ananong, onozea leo katika moyo wa kila mtu, “Sitakuacha peke yako: nitakutumia Roho Mtakatifu. Hata katika upweke wako, nitakua karibu nawe.” [6]

Kuukaribisha utulivu ambao Roho Mtakatifu anatupa kunamaanisha kutafuta, katika kimya na amani, kujitolea kwetu kwake. Hata ingawa kwa wakati mwingine mambo mabaya au ya haraka yanaweza kutokea, ni dhahiri kwamaba tuna weza kuyakabili.

Je, mambo ya tukikasirishwa tunakasirishwa kwa haraka kwa madhumuni ya kutulizwa?

Kuna nyakati zingine ambapo sote tuna shtuliwa na majaribu yetu wenyewe au kwa mateso ya wengine.Hali hii inaweza kuendelea mpaka kuingilia Imani yetu na kuyazima matumaini yetu.Kuugundua tena uaminifu wa imani na amani ya Moyo wakati mwingine inahusisha kujipa wakati.

Aina moja ya mateso huachia haswa alama kubwa: kifo cha mpendwa wetu, kifo cha mtu ambaye tunamtegemea hapa duniani. Lakini majaribu kama haya wakati mwingine yanaweza kubadilishwa sura na kutufungua kuwa uhusiano mwema.

Furaha ya Injili yaweza kumrudia aliye katika huzuni nyingi. Mungu huja na kumwangazia katika siri ya mateso ya mwanadamu, pia hutukaribisha katika uhusiano wa karibu kabisa naye.

Kisha baadaye tunajipata katika njia ya matumaini. Mungu hatuachi pweke, anatuwezesha kuendelea mbele na uhusiano mwema wa imani, uhusiano wa upendo ambao ni Kanisa, kwa wakati na saa moja ni siri ambayo haiwezi kuelezwa kwa maneno……

Katika uhusiano [7] Kristu anatupa zawadi kubwa ya faraja.

Kiasi kwamba Kanisa lina uwezo wa kutuletea uponyaji mioyoni mwetu kwa kutupitishiaa kuihusu msamaha na huruma, inatutengenezea uwezo wa kuwa na uhusiano na Kristu.

Wakati Kanisa linahakikisha kupenda na kuulewa usiri ndani ya kila mwanadamu,wakati kanisa lianatusilikiliza bila kuchoka, kututosheleza kimoyo na kutuponya, inakuwa kwetu ishara ionekanayo. Ni ishara dhahiri ya uhusiano.

Kutafuta msamaha na amani inahusisha nguvu na kujaribi zaidi katika kila mmoja wetu. Haimaanishi ni kuchukua hatua ya kukubali kwa haraka. Hakuna cha kudumu ambacho huja haraka na kwa urahisi. Roho wa uhusiano sio wa kupatitakana kwa harakaThe spirit of communion is not gullible. Husababisha moyo kuhusisha mambo mengi; na makubaliano makubwa na ukarimu hayahusishi mambo yasiyo julikana vyema.

Je, kwa madhumuni ya kuwa watu wa uhusiano mwema, kila mmoja wetu aweza kuendelea mbele na maisha kwa njia ya kuaminiana na moyo wa ukarimu?

Katika njia hii kutakuwa na kutofaulu mara kwa mara.Pia twahitaji kukumbuka kwamba chemchemi ya amani na uhusiano mwema imo ndani ya Mungui.Badala ya kukata tamaa tutamwita Roho Mtakatifu katika udhaifu wetu.

Na katika maisha yetu yote Roho mtakatifu atatuwezesha kuanza upya tena kuanzia Mwanzo mpaka siku za usoni katika amani [8]

Kiasi kwamba jamii yetu huleta uwezekanokatika kukua katika wanadamu....

Ilirekebishwa mara ya mwisho: 1 October 2007

Footnotes

[1Yohana 14:27

[21 Yohana 4:8

[3Isaiya 43:4

[4Wakati wa kulifungua baraza la vijana mwaka wa 1974,Bruda Roger alisema “Bila upendo,ni nini kizuri cha kuishi?Kwa nini kuishi hata zaidi? kwa sababu gani? Hiyo ndiyo maana ya maisha yetu:kupendwa daima,kupendwa milele, ili pia tufike kiasi cha kufa kwa ajili ya upendo.”Heri wanaokuifa kwaajili ya upendo.”Kufa kwa upendo kwake kulimaanisha kupenda mpaka mwisho

[5”Kuishi kama watu waliopatanishwa.”Katika kitabu chake A prospect of Hapiness? Kilichotokea wiki mbili kabla ya kifo chake.Bruda Roger alielezea tena maana ya maneno haya kwake. “Je ninaweza kukumbuka hapa ya kwamba nyanya yangu aligundua ufunguo wa wito katika jumuiya ya Imani na alinifungulia njia ambayo niliifwata kwa matendo? Baada ya vita vya kwanza vya dunia alitamani sana mtu yeyote asikipitie alichokipia yeye.
Kwasababu wakristu walikuwa wakipigana wenyewe kwa wenyewe katika bara la Uropa.aliwaza nakujisemea kwamba ni vyema wakisameheana tena,ili vita vingine visije vikazuka.Alitoka katika familia ya kiprotestanti, lakini aliishi maisha ya jumuiya ya undani, alianza kulihudhuria kanisa la katoliki bila ya kuachana na watu wake.

[6Yohane 14:18 and 16:7

[7“Kristu wa kutuunganisha.” Bruda Roger alikuwa ametumia kielelezo hiki kumkaribisha Baba mtakatifu Yohane Paulo wa Pili katika Taize mnamo mwezi wa Oktoba tarehe tano mwaka wa 1986: “Matumaini yangu na ya ndugu zangu ni kuwa kila kijana amtambue Kristu,sio kristu katika utengano bali Kristu wa kutuunganisha ambaye yuko katika lile fumbo la kutuunganisha ambalo ni mwili wake na kanisa.Hapo vijana wengi wanaweza kupata njia ya kujitolea katika maisha yao hadi mwisho.Hapo wana yote wanayohitaji ili wawe waumbaji wa imani na upatanisho, sio tu kwao bali katika kila kizazi, kuanzia kwa wazee hadi kwa wale wachanga... Katika Jamii yetu ya Taizé, Kumfwata “Kristu wa kutuunganisha “ni kama ule moto ambao unatuchoma tungeenda katika pembe zote za dunia ili tupate njia, tuulize, tusisitize na kuomba kama kuna haja.Lakini kamwe hakuna, ukiwa unaamua kubaki katika ile hali ya kipekee ya umoja ambayo ni kanisa.”

[8Hizi aya nne za mwisho,zilisemwa na Bruda Roger mnamo Disemba 2004 wakati wa mwisho wa mkutano wa bara Uropa mjini Lisbon.Hayo ndiyo maneno yake aliyoyasema mbele ya umati.