TAIZÉ

Alama za picha wakati wa kuabudu

 

Alama za picha huchangia uzuri wa kuabudu. Ni kama madirisha yanayotuwezesha kuona uhalisia wa ufalme wa Mungu, na kuufanya kuwepo katika sala zetu humu duniani.

Japokuwa alama za picha ni taswira, siyo vitu vya maonyesho au mapambo ni zaidi ya hapo. Ni alama zinazoonyesha kitu fulani kikubwa, uwepo ambao hupelekea macho ujumbe wa kiroho ule ule ambao hupelekwa na neno masikioni.

JPEG - 19.1 kb

Kulingana na teolojia ya karne ya nane Mtakatifu ‘John Damascene’, msingi wa alama za picha ni kuja kwa Kristo duniani. Wokovu wetu umehusishwa na neno litokalo kwa Mungu, na vitu. “Zamani Mungu asiyekua na sura, umbo wala kuonekana alikuwa hawakilishwi na kitu chochote. Lakini sasa huyo Mungu ameonekana katika sura ya kibinadamu na amekua kati ya watu, ninawakilisha sura ya mwenyezi Mungu. Siyo kuwa naabudu vitu, la hasha; “Naabudu muumba wa vitu, ambaye amejifanya kitu kwa ajili yangu; ambaye alichagua kuwa kati ya vitu na kwa kupitia vitu, amesababisha wokovu wangu” (‘Discourse’ I,16)

JPEG - 22.3 kb

Kwa imani, kwa uzuri na ukiwa umezama ndani kabisa, alama ya picha inaonyesha uwezekano wa kufanya uwepo wa amani na subira yenye matarajio. Hutualika kupokea wokovu hata katika ubinadamu wetu, na yale yanayo tuzunguka.

Ilirekebishwa mara ya mwisho: 14 August 2007

Ikoni ya Bikira Maria katika kanisa la mapatano, Taizé.

“Hii ikoni ilibarikiwa na Metropolitan Nicodim wa Leningrad, alipoitembelea Taizé mwaka 1962”