TAIZÉ

Barua 2008

Barua kutoka Cochabamba

 
Imetayarishwa kwa miezi na parokia,familia za jijini na mazingira yake,mkutano wa vijana wa amerika ya kusini ulikuwa umeandaliwa huko cochabamba, Bolivia, kutokea Oktoba 10-14, 2007. Iliwaleta pamoja washiriki 7000 kutoka maeneo mbalimabli ya Bolivia, kutoka nchi zote za amerika ya kusini na kutoka nchi za ulaya. Hii “Barua kutoka Cochabamba” ya mwaka 2008 ilisambazwa kwa mara ya kwanza wakati wa mkutano wa ulaya huko Geneva mwishoni mwa Desemba 2007.

Upatanisho ni, kichocheo

Huko Bolivia sisi pamoja na vijana kutoka nchi zote za america ya kusini,tumekuwa tukijiuliza wenyewe: Ni njia zipi za matumaini tunaweza kuzifungua leo? Watu wa Bolivia, pamoja na ukubwa mno wa jamii na wingi wa makabila, wanajaribu kuacha nyuma migogoro na kuelekea kwa ukubwa kwenye haki na amani.

Sehemu nyingi za dunia, kwa sasa migogoro inaibuka kutokana na vidonda vilivyotunga usaha vya kihistoria. Wapi uponyaji unapatikana wakti pale kunahisia za kutokuwa na nguvu na kutokuwa na haki vinaota mizizi?

Mkutano wa vijana huko Cochabamba umeonesha tofauti, badala ya kuongoza kwenye matabaka yenye kusikika kila mara, umebeba ndani yake ahdi ya maafikiano yanayositawi na furaha. [1]

Huko Bolivia, tumegundua kuna waamini wenye moyo wa kufanya wanaloamini kwa kuonesha namna wanavyoyaishi maandiko matakatifu katika kuwa na moyo wa upatanisho.

Katika chemichemi ya upatanisho

Tumetumia nguvu zitakiwazo kw akupigania moyo wa upatanisho ushirika mtakatifu wa mtu binafsi na mungu anayeishi.Bila ya maisha ya ndani, Hatuwezi kuelekea kwenye manuio yetu. Kwa mungu tunapata furaha; Tunapata matumaini ya maisha ya kudumu.

Si mungu mwenye amekuja kwetu sisi? Kwa kuja Yesu, Mungu mwenye amejifanya mtu. Wakati imebakia nje ya uwezo wa kila kitu tunakielewa,mungu amejidhihilisha karibu sana kwa kila moja.

Nje ya upendo, Mungu ametaka kushiriki upo wetu. Amekuwa mtu. Zaidi: kwa kutoa maisha yake juu ya msalaba, Yesu amechagua sehemu yake ya mwisho. [2] Cha kuvutia kutoka kwake ndicho kinatutenganisha sisi kutoka kwa mungu, ana sadiki uumbaji wetu na uanadamu wote. [3] Ametupatia uhai wake kweut sisi. [4] Kwa namna hiyo uumbaji wote ulianza. [5]

Mawasiliano haya pamoja na mungu yanakuwa ya kweli kwetu kwa sala: Kwa Roho mtakatifu,Mungu amekuja kuishi ndani mwetu. Kwa maneno yake na kwa sakramenti, Kristu amejitoa kwetu sisi. Kwa malipo, tujitoe kwake. [6]

Kwa namna hii kristo haja leta kichocheo juu ya dunia, kichocheo hicho tayari kipo ndani yetu?

Kueneza urafiki wetu utawahusisha wote

Hatuwezi kuzuia kichocheo cha upatanisho ndani yake. Inatoa mwanga katika njia kwa wapatanishi wa karibu na mbali. [7]

Kama tutaelewa kwa namna gani mungu anafanya kwa ajili yetu, mahusiano ya maafikiano yangebadilika. Tungekuwa na shauku ya ushirika mtakatifu kwa wengine, kubadilishana maisha ambayo tunatoa na kupokea.

Injili inatualika kuwaelekea wenzetu, bila ahadi yoyote kutoka kwao.

Kwenye hali nyingine,hasa kwenye mahusiano yaliyovunjika,upatanisho unaweza kuonekana hauwezakaniki. Lazima tutambue hali ya kuhitaji upatanisho tayari ni mwanzo wa mapatanisho. Yesu mwenye amejichulia kam hawezi kuongoza chochote na tunaweza kuponywa wote wahitaji. Hicho kinatutayarisha kutumia vizuri nafasi inayoibuka na kuchukua hatua, licha ya udogo lakini tunaelekea kwenye utulivu.

Upatanisho unaweza kugeuza jamii zetu kwa undani. Roho ya kristu mfufuka imebadilisha sura dunia. Acha turuhusu haya mabadiliko ya ufufuko yatupeleke mbele! Tusikate tamaa kutokana na magumu tunayoyakabili. Tusije tukasahau kuwa tunaweza kuanza na kidogo. [8]

Ushirika mtakatifu wa kanisa unatusaidia; ni sehemu ya urafiki wa kila moja. [9] “Kwetu kanisa ni kam Mama anayesikiliza watoto wake. Anawakaribisha; anawafariji.” [10] Haya maneno ya vijana wa amerika ya kusini yametupa changamoto sisi: Je tunatafuta njia y akuruhusu upendo wa kimungu kuonekan kwetu?

Katika hali ya machafuko, je tutatafuta njia ya kusikilizana kwa kila moja wetu? Kwa hiyo mifarakano mbalimbali itakuwa na machungu machache. [11] Acha tupiganie tuwe karibu na wengine.

Je, tutatafuta njia ya kuhakikisha mgawanyo sawa wa maliasili? Acha tuweke hitaji la kufikiria tena kuhusu mtindo katika mwelekeo mkubwa wa unyenyekevu, umoja pamoja na ufukara na kuongeza kuthamini uumbaji.

Je, tutakuwa karibu na masikini kupindukia kiliko sisi? Kwa kushiriki nao, mabadilishano ya kimaisha yanatoa: Wanatuongoza katika ukarimu na kutuweka pamoja nao. Zaidi ufukara unatusaidia kukubali. Kwa kufanya haya tutachangia katika utu wa kila binadamu .

Je, tutaenda kwenye hali ya kusamehana? Je, kuna njia nyingine za kupinga mlolongo wa udhalilishaji unaoendelea? [12] Si kitu cha kusahau yaliyopita, au kuwa wapofu katika hali ya sasa ya kutokuwa na haki. Injili inatuhitaji kwa uwezo wetu kuyakumbuka majereha,kwa kusameheana na kutokuwa na matarajio yanayoibuka katika kupata chochote kama malipo. Kwa namna hii tumetafuta uhuru wa watoto wa mungu.

Ndio, Tunahitajika kupigania pamoja n amoyo wa upatanisho, kwa kuwa watafutaji wenye shauku na ushirika mtakatifu, tuweze kueneza urafiki wetu utakaowahusisha wote.

Ilirekebishwa mara ya mwisho: 16 June 2008

Footnotes

[1Wakati vijana wanawasili kutoka maeneo ya vijijini huko Cochabamba wamevalia mavazi yao ya jadi, ilikuwa ni tamasha la rangi! Ilikuwa yenye furah kuona vijan kutoka maeneo mbalimbali ya Bolivia wankuwa pamoja: wale wanaotoka kwenye tambarare na wale wanaotoka kwenye milima, wale wanaotoka jijini na wale wanaotoka pembeni mwa nchi. Mkutano huu umeonesha ya kuwa vijana wanaweza kuchangia kwa namna ya maisha yao, katika hali ya udharura “wa udogo wa hali ya mapatano.” Kwa kweli injili inakuwa ni nguvu ya mapatano huko Bolivia, ongezeko la wakristu katika kujaribu kutangaza imani kwa kuzingatia zaidi utamaduni na asili ya dini.

[2Kwa mtakatifu Paulo, kwa yeye kuvipatanisha vitu vyote na nafsi yake,akiisha kufanya amani kwa damu ya msalaba wake. Kwa yeye “ikiwa ni vitu vilivyo juu ya nchi,au vilivyo mbinguni” (wakolosai 1:20). Kwa hiyo, “Yesu kristo naye hakuona kule kuwa sawa na Mungu kuwa ni kitu cha kushikamana nacho, bali alijifanya kuwa han utukufu akatwaa namna ya mtumwa, akawa ana mafano wa wanadamu” (wafilipi 2:5-11).

[3Katika lugha ya kimashairi ambayo imechukua mfano wa kuvutia kutoka kwenye tafakari za neno,liturjia ya ki- Orthodox wanaimba kipindi cha Christmas: “Muumbaji,ameona kwamba mtu ambaye mikono yake ilikuwa imepotea , amekuja kuiitisha mbingu; mzaliwa mtakatifu, bikira asiye na mawaa, alisadiki utu wote uko kwenye mwili wake.”

[4Mkristu wa karne ya pili, Irenaeus wa Lyons, alisema: “kwa kuzingatia upendo usio na kikomo,kristu amekuwa kama tulivyo, kujidhihirisha jinsi alivyo.”

[5Roho mtakatifu ni kama roho ya uumbaji: “Uzuri ambao dunia unaonesha unadumishwa kwa kutiwa uzima na roho…. Roho imetawanywa juu ya anga, kuendeleza, kutia uzima, na kuharakisha vitu vyote, pote mbinguni na duniani.” (John Calvin, Institutes of the Christian Religion I, XIII, 14).

[6Ushirika mtakatifu pamoja na mungu si mara zote unapita katika hatua ya hisia; uwepo wa roho mtaktifu ndani mwetu ni mkubwa. Hata kama hatuna hisia yoyote tunaweza kusali, Huenda kwa kutumia ishara: kwa kupiga magoti,kufungua mikono yetu . Na tayari Mungu anakuja kwetu.

[7Yesu akawaambia, njoni mnifuate, nami nitawafanya kuwa wavuvi wa watu. Angalia Marko 1:17.

[8Angalia Luka 10:1-16.

[9Roxana, kijana wa kike wa kibolivia, alielezea jukumu kama kanisa ambalo hutumia katika kujaribu kusaidia kupunguza migogoro ya kijamii ambayo imeisumbua Bolivia: “Ni kitu gani, tia hasira kali na kutia unyonge wa watu? Je, ni ukosefu wa upendo? Unyonge wa wale wote waliojua sauti zao hazisikiki? Wakati unataka kushiriki masumbuko ya watu,unahisi kuwa karibu na matumaini ambayo yanatoka kwa mungu . Kwahiyo na, milango ya makanisa imefunguliwa kwa sala zisizo na mwisho; kengele zinapigwa kualika watu kutoka kwenye vitongoji mbalimbali kwa ajili ya taarifa za mikutano. Vijana wamegungua nguvu ya umoja, kuungana na urafiki. Sisi vijana ni damu ya kanisa; mahudhurio yetu na nguvu zetu ni za lazima.”

[10“Mungu akasema: inawezekana vipi mwanamke akamsahau mtoto wake; si tunda lake lilotoka tumoni mwake? Hata kama atamsahau, sitaweza kuwasahau ninyi” (Isaya49:15).

[11Masikilizano kati ya mtu na mtu ni muhimu katika mahusiano ya watu na jamii kwa ujumla, na hata kwenye mahusiano ya kimataifa kati ya watu na mabara.

[12Kitu cha kustaabisha kwenye mkutano wa huko Cochabamba ni uwepo wa vijana wengi kutoka chile, ambao wana mahusiano ya kiadui kati nchi hizi mbili. Siku ya mwisho wa mkutano, vijana wa kichile walihitaji kujielezea na kuonesha ishara ya upatanisho kwa vijana wa kibolivia,kwa kujieleza kwao, kwa barua ya wazi kwa kuomba msamaha kwa mapigano yaliyotokea na yaliopo kwa sasa.