Inapowezekana, inapendelewa kukutana kanisani, na kupafanya pa kupendeza na kuvutia. Jinsi mahali palivyo andaliwa ni muhimu sana kwa ubora wa sala.
Katika hali ya kawaida siyo lazima kufanya ukarabati wa kanisa lote! Mazingira mazuri ya sala yanaweza kuandaliwa kwa namna rahisi sana. Kama hakuna uwezekano wa kukutana kanisani, ni muhimu kutengeneza mahali pa sala kuwa shwari kadiri mnavyoweza.
Inapendekezwa kuwa wakati wa sala washiriki wote waangalie(wageukie) upande mmoja, kama njia ya kuonyesha kuwa wote tunaelekeza sala zetu kwa kristu na siyo baina ya mtu na mtu.
Sehemu ya sala inaweza kufanywa yenye mvuto kwa kitu kidogo sana; msalaba, biblia iliyofunguliwa, mishumaa, alama za picha, na maua. Mwanga sehemu ya kusalia ni vizuri ukawa wa kufifia na sio mwanga mkali. Unaweza kuweka zulia sehemu ya katikati kwa ajili ya wale wanaopendelea kusali wakiwa wamepiga magoti au wakiwa wamekaa aridhini; Mabenchi au viti, ni vizuri viwepo pembeni kwa ajili ya wale wanaopendelea kusali wakiwa wamekaa juu yake.
Ni vizuri kuwakaribisha watu wanavyoingia, kuwapa karatasi za nyimbo na kuwakaribisha wasogee mbele.
Kwa wengine kuongoza sala ni huduma. Inahitajika kuandaa sala na kuhakikisha inaendelea kwa namna ambayo inamruhusu kila mmoja kwa muda wote kuzingatia yale ya msingi, bila kuvurugwa. Pindi tu sala ikishaanza, kusiwe na matangazo au maelezo ambayo yatavuruga mtiririko.